• Latest News

    June 30, 2016

    Ukawa wavaa nguo nyeusi, wabeba mabango ya ujumbe kwa JPM, Dkt. Tulia

    BUNGE UKAWA (1) BUNGE UKAWA (2) BUNGE UKAWAAA (1) BUNGE UKAWAAA (2) BUNGE UKAWAAA (3) BUNGE UKAWAAA (4) BUNGE UKAWAAA (5) BUNGE UKAWAAA (6) UKAWAA
    WABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani leo asubuhi wameingia bungeni wakiwa wamevalia nguo nyeusi wote walipohudhuria kikao cha 54 cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.
    Baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson kuingia bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge, walianza kunyanyua mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakitoka nje ya ukumbi wa bunge hilo.
    Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma mara baada ya kutoka nje, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia, amesema hawajatoka wala kulikimbia bunge, na kwamba wapo bungeni na wanaendelea kufanya kazi za bunge.
    “Hatujakimbia bungeni, tunashiriki kwenye kamati, hatujasusia bunge, tumechukizwa, tunahasira na vitendo vya kibabe, vya kionevo vinavyofanywa na kiti.” Alisema Mbatia

    CHANZO: GPL
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 maoni:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ukawa wavaa nguo nyeusi, wabeba mabango ya ujumbe kwa JPM, Dkt. Tulia Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
    Scroll to Top