Header Ads

Uwoya Azipa Kisogo Filamu kujikita zaidi kwenye ishu hii hapa


MREMBO aliyejulikana zaidi kwenye Tasnia ya Filamu Bongo kupitia Filamu ya Oprah aliyofanya na marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ pamoja na Vincent Kigosi ‘Ray’, Irene Uwoya amefunguka kuwa kwa sasa ameamua kujikita zaidi kwenye ishu za ujasiriamali kuliko kazi yake ya filamu maana anadhani zitamtoa kimaisha.
uwoya (1) 
Akichonga kwa kujiachia na mwandishi wetu, Uwoya alisema tofauti na kipindi cha nyuma alipokuwa anatumia muda mwingi kukaa na mastaa wenzake wa filamu Leaders Club huku wakisubiri mashavu ya kuigiza muda huo anautumia kusimamia ishu zake za kibiashara.
“Siyo kama nimeacha filamu          hapana, nimeamua tu kujikita zaidi kwenye masuala ya ujasiriamali ili kutanua wigo wa kuingiza kipato, nitakapopata nafasi nitakuwa nafanya filamu kama kawa,” alisema Uwoya.

No comments