Header Ads

WEMA, MADAM RITA WAZUA GUMZO KUBWA!

Gumzo! Kwa mara nyingine, Wema Sepetu ametengeneza habari. Safari hii ni baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bench Mark Production, Rita Paulsen ‘Madam Rita’, ndani ya ukumbi wa Escape One na kusababisha gumzo kubwa. 
 

NI ESCAPE ONE 
Tukio hilo ambalo liliwaacha watu midomo wazi lilijiri Jumamosi iliyopita katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na shoo maalum ya kuadhimisha miaka kumi ya staa wa dansi Bongo, Christian Bella ‘Obama’ ambapo mwandishi wetu alishuhudia tukio mwanzo mwisho. 

MCHEZO ULIVYOANZA
 Awali, Wema aliyeambatana na kruu yake, aliingia ukumbini hapo na kwenda kukaa katika meza iliyokuwa karibu na jukwaa ambapo ni jirani na alipokaa Madam Rita, kila mmoja kwa wakati wake akipata ‘kilaji’ huku wakitazama shoo mbalimbali za utangulizi.
 

SHOO YANOGA 
Kutokana na shoo hiyo kuwa ya kihistoria, wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva kama Ben Pol, Maua Sama, Barakah Da Prince na Dully Sykes walishambulia jukwaa vilivyo kabla Bella hajapanda hivyo kusababisha mamia ya watu waliofurika ukumbini hapo wakiwemo Wema na Madam Rita kulipuka kwa shangwe. 

USHUHUDA WA KUCHANGAMKA
 Wakati Wema na Madam wakiendelea kupata mambo yao, huku muziki mzuri ukiendelea kupigwa jukwaani, mpenda ubuyu mmoja aliyewaona wawili hao, alimdokeza mwanahabari wetu kuwa mastaa hao wamefi kia patamu, wamechangamka. 

“Enheee, ndiyo ndiyo… naona sasa mambo yamekuwa mambo. Madam Rita kachangamka kweli. Wema ndiyo balaa. Wanayumbayumba kufuata mapigo ya muziki,” alisema mdaku huyo. 

BELLA APANDA JUKWAANI
 Baada ya wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva ‘kulisafi sha’ jukwaa, mwenye shughuli yake, fundi wa sauti, Bella alipanda jukwaani na baada ya kuamshaamsha mashabiki kwa kuimba ‘akapela’ ndipo alipomuita Wema ili kwenda kufungua shampeni na kukata keki kama ishara ya uzinduzi rasmi wa sherehe hiyo. 

WEMA AMUONA MADAM, AMPA HI 
Wakati Wema akielekea jukwaani kwa mwendo wa ‘mbili mbele, mbili nyuma’ kutokana na kuonekana kuzidiwa na kinywaji, alipita katika eneo alilokuwa amesimama Madam Rita na kumsalimia lakini akashindwa kuzungumza naye kwa kirefu kwani alikuwa akihitajika jukwaani. 

ASHINDWA KUPANDA NGAZI 
Alipofi ka katika ngazi za jukwaani, Wema alishindwa kupanda ngazi akiwa amevaa viatu virefu, akalazimika kuvivua na kwa msaada wa msanii mwenzake aliyeambatana naye, Esha Buhet, alifanikiwa kufi ka jukwaani na kufungua shampeni kisha zoezi la kukata keki likafuatia.
 

WEMA AWA WA KWANZA KULISHWA 
Baada ya Bella kukata keki, alimlisha Wema, akafuatia aliyekuwa mbunge wa Urambo Magharibi, Juma Kapuya, ambaye alikuwa mmiliki wa Akudo Impact ‘vijana wa masauti’ bendi iliyompatia umaarufu,  kisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wadau wengine. 

WEMA AREJEA KWA MADAM
 Baada ya matukio hayo, Wema alishuka jukwaani na kwenda moja kwa moja kwa Madam Rita, wakakumbatiana kwa muda huku kila mmoja akionekana ‘kummisi’ mwenzake. 

WAGANDANA
Kuonesha kweli wamemisiana, wawili hao walibusiana midomo na kutulia kwa sekunde kadhaa huku Madam Rita akiwa amemshika kwa hisia Wema kiunoni hali ambayo iliwafanya jamaa waliokuwa jirani yao kuzua gumzo.

 “Mh! Huu uzungu  sasa umezidi, mastaa wana mambo hawa, haya yetu macho,” alisikika shuhuda mmoja akisema huku watu zaidi waliokuwa karibu wakiwasogelea na kila mmoja kusema lake. 

WAACHANA
Baadaye wawili hao waliachiana na kila mmoja kuendelea na starehe zake huku wakiinjoi muziki mzuri kutoka kwa Bella. Mwisho wa shughuli, kila mmoja aliondoka kivyake.

CHANZO: RISASI JUMATANO

No comments