Header Ads

Wizkid na Diamond wameipoteza tuzo ya BET Mshindi ni Black Coffee wa Afrika Kusini


Mshindi wa BET Awards 2016, kipengele cha Best International Act: Africa ni Black Coffee wa Afrika Kusini.
image
Ushindi wake umeshangaza wengi. Waliokuwa wanatarajiwa zaidi kushinda tuzo hiyo ni Diamond na Wizkid. Na kwa mashabiki wengi wa Diamond, Wizkid ndiye waliyekuwa wakimhofia zaidi. Lakini tulikuja kujipa moyo kuwa huenda mwaka huu ushindi ni wetu kutokana na msimamo wa Wizkid dhidi ya tuzo hizo za Wamarekani.
Mwaka jana alieleza sababu ya kutohudhuria akidai kuwa haziwapi heshima wasanii wa Afrika na UK. Na tangu atajwe kuwania tuzo hizo, hajawahi kujali,  kusema chochote na hakuhudhuria kabisa. Hivyo nafasi kubwa ilionekana kwenda kwa Chibu. Hata hivyo, BET waliamua kumpa Black Coffee – Dj ambaye jina lake ni geni kabisa kwa Watanzania wengi.
image
“For the past 4/5 years I have been doing tours outside my Country…..in the last two years even relocating my Family with me while on tour to make everything work…..Taking our South African Music to places I can’t even pronounce,” aliandika kwenye Instagram baada ya ushindi huo.
“I’m Greatful to my lady @enhlembali_  and my kids for allowing me to chase my dreams unconditionally…….my great team @amarudacosta @lionelmarciano and both offices in SA and NY….Universal Music team in SA…..Ultra Music team in NY and the William Morris Team in LA…..a BET  Award comes to our our Land for the first time.This is a Great Honour…..We did not do this alone…Thank you for all your Votes…..Thank you for the Love. #betawards16 #bestinternationalaact2016 #gotnothingbutloveformypeople #southafica #onemanband #Godsveryown #california #itsallpossible,” aliongeza.
Diamond alimpongeza pia kwa ushindi huo. Lakini pamoja na jina lake kutokuwa kubwa katika upande mwingine wa Afrika, ukitoa Kusini, Black Coffee ni legend ambaye katika wote aliokuwa ametajwa nao, yeye ndiye kaka yao.
Black Coffee ni nani?
image
Jina lake halisi ni Nathi Maphumulo. Ni Dj mwenye mkono mmoja. Alipoteza mkono wake baada ya taxi kuanguka kwenye kundi la watu ambalo naye alikuwemo, mtu mmoja alikufa na Black Coffee alikuwa mmoja wa watu 36 waliojeruhiwa.

No comments