Header Ads

Wolper atibua tafrija ya staa mwenzake Shilole atinga na Bilauri!

 
Mkali wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper Massawe, wikiendi iliyopita alidhihirisha uhai wa jina lake la ‘Wolper Gambe’ baada ya kutibua tafrija ya staa mwenzake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ aliyefuturisha nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar. 

WIKIENDA NDANI YA NYUMBA 
Katika futari hiyo ambayo Wikienda lilikuwa ndani ya nyumba, ilikusanya mastaa mbalimbali wa Bongo wakiwemo Shamsa Ford, Jini Kabula, Esha Buheti, Flora Mvungi, Nisha, Dude, Niva, Kunguru, Wolper, Davina, Thea, Fredy wa Makomandoo na wengine kibao. Katika hali iliyowashangaza wengi ni kitendo cha Wolper kutinga akiwa ‘amegambeka’ jambo lililowatibua baadhi ya wasanii na wahudhuriaji.

WOLPER ATINGA NA BILAURI 
Wolper alitinga katika tafrija hiyo akiwa na bilauri ya plastiki yenye rangi ya dhahabu huku ndani yake kukiwa na kinywaji ambacho baadaye ilibainika kuwa ni ‘ulabu’ ingawa haikuwa rahisi kujua ni aina gani ya ‘mambo’. 


WASANII WANONG’ONA Baadhi ya wasanii walisikika wakinong’ona baada ya kumuona Wolper akiwa na harakati ambazo si za mtu mwenye akili yake binafsi kwani alionekana ‘kuchangamka’ kupita kiasi. “Wasanii wakati mwingine tunajidhalilisha wenyewe, Wolper anaonekana kalewa kabisa ndiyo maana unamuona anaongea na kucheka sana. Si akili yake, hiyo ni ya mtungi, hata hivyo kama si kutibua shughuli ya mwenziye ni nini?” Alisikika mmoja wa wasanii wakubwa wa sinema za Kibongo anayejiheshimu. Jambo hilo liliwafanya waandishi wetu kuwa makini na kuanza kumfuatilia Wolper hatua kwa hatua. 

FULL SHANGWE Katika hali ya kawaida, Wolper alikuwa tofauti na siku nyingine au akiwa hajaonja ‘maji ya dhahabu’ kwani huwa ana aibu lakini kwenye shughuli hiyo, aibu ilikwenda likizo kwani alikuwa akipiga shangwe la kufa mtu. 

AMKUMBATIA SHILOLE NA WENGINE Baada ya kumaliza kufuturu, Wolper
alinyanyuka akiwa na glasi yake kisha akaenda kumkumbatia Shilole kwa kumpa hongera ya futari pamoja na wasanii wengine. 


MAPICHAPICHA NA WAHUDHURIAJI Akiwa ni mwingi wa furaha, msanii huyo alionekana kupagawa na zoezi zima la kupiga picha na wasanii wenzake pamoja na mashabiki waliohudhuria. Mbali na Wolper, wasanii wengine waliopata majanga ni: 

DAVINA APOTEZA SIMU “Futari ilikuwa nzuri sana ila mimi imeniacha na maumivu makali kwa kupoteza au kuibiwa simu yangu, ishu siyo simu sema namba na taarifa zangu zilizomo,” alisema Davina. 
FLORA MVUNGI AKOMBWA VIATU Kutokana na watu kuwa wengi, msanii mwingine wa filamu Bongo, Flora Mvungi alikombwa viatu vyake kwenye futari hiyo huku kukiwa na malalamiko kwa baadhi ya wahudhuriaji kuibiwa vitu vyao kama ilivyotokea kwa mastaa hao. 
SHILOLE ATANGAZA KUSOMA ALBADILI Kutokana na wahudhuriaji na wasanii kuibiwa vitu vyao, Shilole alitangaza kuwa walioiba warudishe laa sivyo ataporomosha Albadili (Kisomo cha Kiislam cha kuwashitakia wezi kwa Mungu). “Jamani aliyeona simu, viatu na vitu ambavyo siyo vyake namuomba arudishe, siyo vizuri na kama hatarudisha Albadili inamhusu,” alisema Shilole na kuongeza: “Kwa yeyote aliyeibiwa au kupoteza kitu chake aje aniambie nitawalipa kwa sababu mimi ndiye niliyewaalika ila poleni sana.” ‘
VYUKU’ VYA KUTOSHA “Kiukweli futari ya Shilole ilikuwa ni baab’kubwa, ‘vyuku’ vya kutosha sana, watu tumekula hasa, kiukweli nimesaza,” alisema mmoja wa wasanii aliyeomba ahifadhiwe jina. 
DUDE AIBUKIA JIKONI Mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ aliyechelewa kufika, alipitiliza moja kwa moja jikoni na kuchukua sahani yake ya futari iliyokuwa imesheheni njugu, magimbi, maboga, nyama na vinginevyo. Mbali na yote, maandalizi ya futari hiyo yalikuwa mazuri kwa kila idara.

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA

No comments