Header Ads

Amber Lulu adaiwa kusitiriwa msiba wa mama yakeUntold story! Kufuatia nguo zake za vichupi anavyovaa wakati mwingi, video queen maarufu Bongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ ililazimika asitiriwe na majirani siku ya msiba wa mama’ke kwa kumrushia kitenge.
Kwa mujibu wa sosi wetu, tukio hilo lilijiri miaka kadhaa iliyopita mkoani kwao Mbeya ambapo Amber Lulu alitoka kujirusha Klabu ya Vibes ambayo kwa sasa ni Maisha na kukutana na msiba wa mama’ke.
Chanzo hicho kilidadavua kwamba, mzazi huyo aliugua kwa muda mrefu ambapo wakati anakutwa na umauti, Amber Lulu alikuwa amekwenda klabu hivyo aliporejea akiwa nusu utupu ndipo majirani hao wakamstiri.
Baada ya kumwagiwa ubuyu huo, Wikienda lilimsaka Amber Lulu na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka:
“Unajua watu wakishakuona unatoka na huenda ukawa staa, huwa wanataka kukuharibia. Niseme ukweli kuwa suala hilo ni la uongo kwani siku mama yangu alipofariki dunia nilikuwa naye hospitalini.”

Stori: Wikienda
DAR ES SALAAM:

No comments