Header Ads

Amber Lulu; Kama ana ngoma, watakufa wengi


Stori: Hamida Hassan, Ijumaa
Dar es Salaam: Video Queen anayekuja kwa kasi Bongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ anadaiwa kuwa na msururu wa wanaume aliotoka nao huku ndani yake wakiwemo mastaa kibao, Ijumaa limenyetishiwa.
Shosti wa Amber Lulu aliyeomba jina liwekwe kapuni alisema kuwa, kutokana na figa yake, mdada huyo amekuwa akisarandiwa na midume kibao na kila anayekuwa naye akimuacha, anahamia kwa mwingine.
“Yule Amber Lulu muoneni hivihivi, figa yake asipoitumia vizuri itampoteza maana wanaume wanamshobokea kweli, sijui ni lile zigo (kalio) lake au ana kizizi maana listi yake ya wanaume ni noma, wapo mastaa kibao (anawataja kwa majina) kiasi kwamba kama ana ngoma basi wengi watakufa,” alisema mnyetishaji huyo.
Ili kujua ukweli wa taarifa hizo, paparazi wetu alimvutia waya Amber Lulu na kumuuliza kama anakumbuka idadi ya wanaume aliotoka nao hadi sasa ambapo alidai kuwa hakumbuki ila akakiri kuwa mbali na watu wengine alishawahi kuwa kwenye uhusiano pia mastaa wanne, akiwemo Raheem Rummy ‘Bob Junior’.
“Hao mastaa unaonitajia ni kweli nilishawahi ku-date nao ila kwa sasa nina maisha yangu mengine,” alisema kwa kifupi Amber Lulu ambaye a.k.a yake hiyo imetokana na kufanana kimuonekano na modo wa Marekani, Amber Rose.
Kufuatia mwanadada huyo kukiri kuwa alishawahi kutoka na mastaa mbalimbali, watatu ambao aliwataja hawakuweza kupatikana hivyo majina yao yanaendelea kuhifadhiwa ila Bob Junior alipoulizwa alikana kutoka na binti huyo licha ya kwamba anamjua na alikuwa karibu naye.

No comments