Header Ads

Bamboo: Diamond hana hadhi kutoka na Victoria Kimani


Victoria Kimani.

TASNIA ya muziki Afrika Mashariki ilianza kumfahamu mkali wa miondoko ya Hip Hop, kijana mzaliwa wa Kenya aliyekulia Mitaa ya Inglewood, Califonia, Marekani, Simon Kimani ‘Bamboo’ mwanzoni mwa miaka ya 2000 baada ya kutoa ngoma yake iitwayo Usilete Compe.
Hata hivyo, mkali huyo mwenye mafanikio makubwa katika Tasnia ya Muziki Kenya, ametoa albamu zaidi ya tatu na kwa mujibu wake, iliyofanya vizuri zaidi inaitwa Nairobiszm, aliyoiachia mwaka 2004.

Hivi karibuni Bamboo amefanya ‘Exclusive interview’ na gazeti hili dairekti kutoka ‘Code’ namba 254, Kenya na kufunguka mambo mengi kuhusu kazi yake ya muziki na mambo mengine mengi. Huyu hapa anakuja.
Risasi Vibes: Makazi yako hasa ni wapi, Nairobi au Marekani?
Bamboo: Kwa sasa ni Kenya, nimerudi hivi karibuni, Marekani nitakuwa nakwenda kwa shughuli zangu za kibiashara ambazo nafanya!
Risasi Vibes: Shughuli zipi hizo?
Bamboo_Dueces 
Simon Kimani ‘Bamboo’
Bamboo: Nje ya muziki nafanya biashara. Namiliki ‘bland’ ya mavazi iitwayo Jamhuri Wear, mavazi yangu yanavaliwa na mastaa wengi Marekani, Jay Z anavaa, Akon na wengine wengi. Lakini pia tofauti na mavazi kuna mambo mengi ninafanya.
Risasi Vibes: Umefanya muziki kwa muda mrefu, kitu gani ambacho hutakisahau katika kipindi chako chote?diamondDiamond.
Bamboo: Shoo niliyopiga Bongo mwaka fulani sikumbuki vizuri, kwenye Tamasha la Fiesta. Watu walikuwa ni wengi mno na jambo ambalo sikuamini ni namna walivyokuwa wanatembea na ngoma zangu.
Risasi Vibes: Vipi kuhusu kundi lenu la K-South, lilivunjika?
Bamboo: Dah! Mazee, niliyekuwa naunda naye kundi, Abbas kwa sasa hayuko kwenye gemu tena kiivo, maana ameshakuwa na majukumu ya kifamilia. So lipo kama halipo, lakini tukipata muda tunaweza kufanya kazi pamoja.
Risasi Vibes: Kuna kipindi ulikuwa katika bifu na rapa Octopizo, chanzo chake kilikuwa nini na mliishia wapi?
Bamboo: Of couse Octopizo alikuwa na bifu na Abbas, kila mmoja akijiona rapa mkali. Mimi nilikuwa ninajaribu kuleta tu peace kati yao, sasa Octo akapaniki kuona naingilia, ndiyo maana akaanza kuvuruga kwenye mitandao kwa kuandika maneno machafu juu yangu. Lakini haikuwa bifu kiivo, maana tuliimaliza ukizingatia yeye ni mdogo sana hasa kimuziki kulinganisha na sisi.
Risasi Vibes: Rapa gani unamkubali Kenya?
Bamboo: Wapo wengi lakini kwa hawa walioibuka siku hizi kuna Rabbit
na Kaligraph Jones.
Risasi Vibes: Msanii gani umewahi kuvutiwa kufanya naye kolabo na bado hujafanikiwa kufanya naye?
Bamboo: Namtamani sana Yossou Ndour, hata hivyo bado nipo kwenye gemu siku moja nitafanya naye tu kazi.
Risasi Vibes: Umewahi kutangaza kuwa umeokoka na ukabwaga chini muziki huku ukisema, Hip Hop ni ya ‘Kiilluminate’, lakini umerudi tena na hivi karibuni umefanya kolabo na Prezzo ya ngoma iitwayo Za Ovyo. Unawaambia nini wapenzi wa kazi zako juu ya hili?
Bamboo: Ha! Ha! Haa! Swali zingine hapa noma mazee! Muziki ni muziki na
mambo ya kishetani. Hivyo basi, sipendi kuongeza lolote lile zaidi ya hayo.
Risasi Vibes: Msanii Diamond Platnumz aliwahi kuhusishwa kutoka kimapenzi na dada yako, Victoria Kimani na wewe ukaibuka na kusema hana hadhi hiyo! Nini kilikusukuma kusema hivyo?
Bamboo: Hakuna kilichonisukuma lakini nilisema ukweli. Hana hadhi ya kutoka na Victoria, dada yangu yuko katika levo zingine.
Risasi Vibes: Mbali na Victoria kuna ndugu yako mwingine anafanya gemu la muziki?
Bamboo: Yap, kaka yetu anaitwa Kimya.
Risasi Vibes: Mipango ya kazi mpya vipi kwa sasa?
Bamboo: Bado mimi na Prezzo tunapushi ngoma yetu iitwayo Za Ovyo, hivi karibuni tunatarajia kuja mpaka Bongo kwenye media tour, so baada ya hapo naweza kusema lolote.

CREDIT: GPL -Makala: Boniphace Ngumije

No comments