• Latest News

  July 04, 2016

  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) yakanusha Taarifa kuwa Haina Fedha za kulipa wanafunzi


  TAARIFA KWA UMMA
  KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwa sasa kwamba haina fedha.

  Si kweli kwamba Bodi haina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.

  Hata hivyo, maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

  Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.

  IMETOLEWA NA:
  KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
  BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
  TAREHE 2 JULAI 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) yakanusha Taarifa kuwa Haina Fedha za kulipa wanafunzi Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top