Header Ads

Bozi: Wa ku-date na mimi ajipange sana

 
MSANII wa filamu Bongo ambaye pia anauza nyago kwenye video mbalimbali za wanamuziki, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema kutokana na maisha yalivyo, mwanaume anayetaka ku-date naye lazima ajipange sana.
 
 Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Bozi alisema yeye kama msichana anayekwenda na wakati hawezi
kukubali kujiweka kwa mwanaume kapuku kwa kuwa, ikiwa hivyo lazima atachepuka tu. “Unajua sababu ya wasichana wengi kusaliti wapenzi wao ni kutotimiziwa na wapenzi wao, unaweza kukuta unahitaji hiki,
ukimwambia baby wako anakuambia hana kitu, anatokea mtu anakuambia sema unachotaka unadhani kwa maisha ya sasa utakataa, lazima utasaliti tu,” alisema Bozi.

No comments