• Latest News

  July 26, 2016

  Dayna akana kutoka na Billnas

  DaynaStori: Uwazi Showbiz
  STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amemfungukia staa wa Hip Hop Bongo, Billnas kuwa hakuna uhusiano wowote wa kimapenzi unaoendelea kati yao zaidi ya kazi ya kimuziki.
  BILNAS BILLNAS CHAFU POZI GREGORY ALLSTARTZ DAR MULTITECH ZONEAkichonga na Uwazi Showbiz, Dayna anayebamba na Ngoma ya Komela alisema kuwa awali hakuwa akimjua Billnas lakini baada ya kumuona kwa mara ya kwanza kipindi cha nyuma  katika Studio za Free Nation kwa Prodyuza T. Touch ndipo walipoanza kujuana.
  “Siku moja nilimpigia simu, alikuwa Sauz (Afrika Kusini) kwa shughuli zake za kisanii, nikamwambia nahitaji kufanya ngoma naye. Alikubali na kuanzia hapo tukawa karibu ila kikazi tu, yeye ana uhusiano wake na mimi kivyangu,” alisema Dayna.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Dayna akana kutoka na Billnas Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top