• Latest News

  July 28, 2016

  EXCLUSIVE: SIMBA YAMRUDISHA LOGARUSIC JIJINI DAR ES SALAAM, APEWA KAZI YA KUIPIMA UWEZO


  Kocha Zdravko Logarusic anarejea jijini Dar es Salaam, safari hii akiwa amepewa kazi ya kukipima kikosi cha Simba.

  Logarusic maarufu kama Loga, anakuja nchini ndani ya siku chache akiwa ameongozana na kikosi chake cha Inter Club cha Angola.

  Kikosi hicho kitapambana na Simba katika mechi ya Simba Day ambayo itapigwa Agosti 8, siku ambayo Simba itauwa inatimiza miaka 80.


  Tayari Logarusic alikuwa amesema angetamani kukutana na Simba na kuwaonyesha kazi yake ilivyo bora.

  Sasa Simba inanolewa na Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon na imejichimbia mjini Morogoro.

  Chini ya kocha huyo, Simba imecheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Polisi Morogoro iliyo daraja la kwanza na kuivurumisha kwa mabao 6-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: EXCLUSIVE: SIMBA YAMRUDISHA LOGARUSIC JIJINI DAR ES SALAAM, APEWA KAZI YA KUIPIMA UWEZO Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top