Header Ads

Haitham aumizwa na Madj, watangazaji wa Bongo!

MSANII wa kike anayepanda kwa kasi kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva Bongo, Haitham Ghazal Seif ‘Haitham’ ambaye pia yuko chini ya Lebo ya MJ Records, amesema kuwa changamoto anazokutana nazo wakati mwingine anapokuwa anasukuma kazi zake za muziki kwenye media hasa  kutoka kwa baadhi ya watangazaji na Madj huwa zinamuumiza sana japo hazimkatishi tamaa.


Akichonga na mtandao wa Global Publishers, Haitham aliongeza kuwa kazi kubwa ya kupushi ngoma zake hufanywa na  menejimenti yake lakini pale anapokuwa anaingia mstari wa mbele kwa upande wake hujikuta akikumbana na changamoto hizo ambapo ni pamoja na kuombwa penzi.
“Japo menejimenti yangu inafanya kazi kubwa kuhakikisha ninapiga hatua zaidi kimuziki lakini  ukweli ni kwamba haiwezi kufanya kila kitu, sasa ninaposaka chansi mwenyewe nakutana na changamoto hizo za unyanyasaji wa kijinsia. Ukweli zinatuumiza sisi wanamuziki wa kike jambo ambalo wahusika wanatakiwa kuachana nalo ikiwa ni pamoja na kutuheshimu,” alimaliza Haitham.

CREDIT: GPL-UWAZI

No comments