Header Ads

HENRY AACHIA NGAZI ARSENAL, ILIKUWA NI BAADA YA WENGER KUMWAMBIA ACHAGUE UKOCHA AU UCHAMBUZI KWENYE RUNINGA


Thierry Henry ameamua kuachia ngazi ya ukocha wa vijana katika klabu ya Arsenal.

Gwiji huyo wa Arsenal, ameamua kuondoka katika klabu hiyo baada ya Kocha wake, Arsene Wenger kumwambia achague moja, Arsenal au kuendelea kufanya kazi ya uchambuzi Sky Sports.

Wenger amemueleza Henry kwamba haitakuwa sahihi, katikati ya wiki anakuwa kazini Arsenal halafu wikiendi anakuwa kwenye runinga ya Sky Sports akiwaponda wachezaji wake.

Kutokana na uamuzi huo wa Wenger, Henry anaonekana ameamua kufuata mkataba mnono alioingia na Sky Sports.No comments