• Latest News

  July 24, 2016

  HOFU YAREJEA TENA OLD TRAFFORD, MOURINHO AGAWA MAKUNDI MATATU


  Wakati kocha Jose Mourinho akipambana kumnasa Paul Pogba, inaonekana wazi kuwa kiungo mkongwe Bastian Schweinsteiger ataongoza kundi la ambao watatemwa.

  Tayari Mourinho amefanikiwa kumsajili mshambuliaji mkongwe, Zlatan Ibrahimovic pia  Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan ambaye pia ni kiungo, hivyo nafasi ya Schweinsteiger inakuwa ndogo.

  Lakini kuna wengine walio kwenye hofu ya kutupiliwa mbali ingawa bado kuna viungo watakuwa na nafasi kama Morgan Schneiderlin, Michael Carrick, Ander Herrera na Marouane Fellaini. 

  Wako wenye hofu kama Marcos Rojo, Juan Mata, Matteo Darmian, Memphis Depay, Adnan Januzaj na Ashley Young ambao inaonekana wanaweza kubaki lakini hawana uhakika wa asilimia mia.

  Uhakika wataondoka:
  Bastian Schweinsteiger
  Marcos Rojo 
  Matteo Darmian

  Bado hawana uhakika 50/50:
  Juan Mata 
  Memphis Depay 
  Adnan Januzaj
  Ashley Young

  Uhakika wanabaki Old Trafford:
  Marcus Rashford
  Guillermo Varela 
  Will Keane
  James Wilson 

  Tyler Blackett
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HOFU YAREJEA TENA OLD TRAFFORD, MOURINHO AGAWA MAKUNDI MATATU Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top