Header Ads

Huyu Ndiye Mpenzi Mpya wa Shamsa Ford?

Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford amezua minong'ono katika mitandao ya Kijamii baada ya kuachia picha zake akiwa na mtu anayedaiwa kuwa mpenzi wake mpya. Katika picha aliyotupia katika akaunti yake Instagram juzi Jumamosi, Shamsa alionekana akiwa pembeni ya mtu huyo ambaye hakumuonyesha sura na kuwatakia usiku mwema mashabiki wake. Siku hiyo hiyo baadaye, Shamsa alitupia tena picha nyingine akiwa amelala na mtu huyo aliyekuwa kifua wazi ambapo hakumuonyesha tena sura yake na kuisindikiza picha hiyo kwa maneno yafuatayo; "Kuna muda unaweza ukafanya kitu mtu akakuona mshamba au limbukeni. Ila ukweli ni kwamba hakuna mtu anaweza jua hisia za mwenziye anavyojisikia kwa wakati ule zaidi ya yeye mwenyewe. .TUHESHIMU HISIA ZA WENZETU. ...I love you a man of my dream...NICE Saturday"
G9t my people A photo posted by shamsa Ford (@shamsaford) on
Staa huyo ambaye alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki wa Hip Hop, Nay Wamitego hakuishia hapo ambapo jana aliachia tena picha nyingine akiwa na jamaa huyo na kuficha tena sura yake jambo ambalo bado linaibua maswali mengi kama ndiye shemeji yetu mpya au la. Mashabiki wa staa huyo wengi wameonyesha shauku ya kutaka kumjua mtu huyo ambaye haonyeshwi sura huku wengine wakidai ni Nay mara wengine wakisema ni Raymond kutoka WCB.  
A photo posted by shamsa Ford (@shamsaford) on

No comments