Header Ads

Izzo: Mpenzi wangu hahofii ukaribu wangu na Abela


Emmanuel Simwenga ‘Izzo Bizness’ na Abela Kibira ‘Abela Music’.
MAKALA: Boniphace Ngumije
THE Amaizing ni moja ya makundi ya muziki mapya kwenye Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva ambayo yanavuma kwa kasi mno.
Kundi hili limeanzishwa na ‘kichaa’ wa kurap anayewakilisha masela wa Mbeya City, Emmanuel Simwenga ‘Izzo Bizness’ na mwanadada Mtanzania ambaye mama yake ni Mmarekani, Abela Kibira ‘Abela Music’.
Katika safu hii ya Burudani Mwanzo Mwisho (BMM), Izzo, anafunguka namna alivyokutana na Abela Music, walivyopata wazo la kuanzisha kundi na mipango yao ya kikazi.
izzo (2)BMM: Abela Music ni msanii mpya kwenye gemu, ametoka wapi, mmekutana vipi na ilikuwaje mpaka ukaamua kufanya naye kazi?
BIZNESS: Abela ana asili mbili, baba yake ni Mtanzania na mama ni Mmarekani na amekuwa akiishi nje kwa muda mrefu.
Kwa mara ya kwanza nimekutana naye kwenye mitandao ya kijamii maana ni mfuatiliaji mzuri wa kazi zangu. Akaniambia pia ni msanii, tukaanza kutumiana kazi na nikagundua kuwa ni mkali na tukapanga akirudi Bongo tufanye kazi pamoja.
BMM: Sawa, kufanya kazi ni jambo moja na kuanzisha kundi ni lingine? Nini kilikusukuma hasa mpaka ukafikia kwenye uamuzi huo?
BIZNESS: Swagga zake tu. Ni mkali, niliona ni mtu muhimu kufanya naye kazi kwa karibu zaidi na tukichanganya ladha yake na yangu, mashabiki watapata kitu kizuri sana.
izzo (1)BMM: Uliwahi kuwa na mawazo ya kuanzisha kundi kabla ya kukutana na Abela?
BIZNESS: Yeah, time tu ilikuwa haijafika na kila kitu hupanga Mungu, nafikiri alikuwa amemuandaa Abela kwa ajili ya kufanya kazi na mimi!
BMM: Mbali na nyie wawili kuna wengine ndani ya kundi?
BIZNESS: The Amaizing ni zaidi ya Bizness na Abela. Kuna timu kubwa sana japo wengine hawajawa official. Jambo lingine
 ambalo mashabiki wangu wanatakiwa kufahamu, baadaye tuna mpango wa kufanya kundi hili kuwa kampuni.
izzo (3)BMM: Tuzungumzie idea ya jina, The Amaizing, ilitokana na nini na nani aliitoa?
BIZNESS: Tulipopata mawazo ya kuanzisha kundi, tulikaa mimi, Abela na timu yetu nzima, kutafuta jina lipi tutumie. Baada ya kujadiliana tulipata majina matatu na kati ya hayo tulipitisha hili.
Sababu ya kupitisha ni kwamba jina lina swagga, linaeleweka na linaendana na wakati.
BMM: Abela hazungumzi lugha ya Kiswahili sana, ni Kiingeleza mwanzo mwisho, kwa soko la Tanzania huoni kama inaweza kuwa tatizo kuliteka kwa haraka?
BIZNESS: Kama Watanzania wanaweza kusikiliza kazi za wasanii wa nje wanaoimba lugha tofautitofauti ambazo zingine ni vigumu kuzielewa haiwezi kuwa shida kwa Abela. Hata hivyo yeye ni mwanamuziki, haimaanishi kuzungumza Kiingereza tu hawezi kuimba kwa Lugha ya Kiswahili.
BMM: Tetesi za kuwa unatoka naye kimapenzi zimekaaje?
BIZNESS: Hazina ukweli. Mimi na yeye kinachotuunganisha ni kazi, nina uhusiano wangu, naye ana wake pia.
BMM: Kuwa naye karibu sana hakuathiri lolote kwenye uhusiano wako?
BIZNESS: No, ninamshukuru Mungu mpenzi wangu ni mtu mwelewa. Hahofii ukaribu wangu na Abela.
BMM: Kwa kumalizia tu, unawaambia nini wapenzi wa kazi zako kuhusu The Amaizing?
BIZNESS: Tumekuja kufanya mapinduzi kwenye gemu la Muziki Bongo. Ngoma yetu ya Dangerous Boy ambayo tumeachia hivi karibuni inaweza kuthibitisha juu ya hilo. Mashabiki waendelee kunipa sapoti!

No comments