• Latest News

  July 01, 2016

  Kajala aeleza mzimu wa kifo unavyomtesa

  MSANII maarufu wa filamu Bongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa, maisha yake ya sasa hayajatawaliwa na furaha kwani anaona kama vile siku zake za kuishi duniani zinakaribia kuisha. Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Kajala alisema kuwa amefikia hatua ya kusema hayo kwa kuwa, kila wakati moyo wake unamuenda mbio na wakati mwingine kukumbana na ndoto mbaya zinazomfanya aogope.
   

   “Niseme tu kwamba sina amani kwa sasa kwani nakiona kifo changu, nikilala usiku nasumbuliwa na mzimu wa kifo, nikitaka kusafiri moyo unanilipuka, nahisi itakuwa ndiyo safari yangu ya mwisho, wakati mwingine naahirisha safari kwa hofu.

   “Nikiumwa kidogo tu nakosa amani kabisa, naona kama vile sitapona kikubwa namuomba Mungu aniondolee hali hii ndiyo maana nimekuwa mtu wa ibada muda mwingi,” alisema Kajala
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Kajala aeleza mzimu wa kifo unavyomtesa Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top