Header Ads

Kanga Moja Kiunoni... MBENGEMBEGE-16ILIPOISHIA : Mama Mei na mzee Hewa walisimama mlangoni wakiangalia uwezekano wa kutoka kwani aliyekuwa akigonga alikuwa kama ameondoka... “Ngoja nitoke mimi halafu wewe utafuatia ili nikaangalie mazingira kwanza,” alisema mzee Hewa... TAMBAA NAYO SASA...“POA.” Mzee Hewa alifungua mlango, akatoka kwenda chooni kisha akaenda mpaka nje, mbele ya nyumba yake hiyo, kote akaona kuko kimya, hakukuwa na dalili yoyote ya watu kuwepo eneo hilo. Hata nyumba za majirani pia zilipoa. Akapita mlango kwa mlango ndani kwake kuhakiki kama kuna mpangaji yumo ndani. Akafika kwenye mlango wa kuingia kwa Mfaume, akaona pia umefungwa tena na funguo, akarudi ndani kwake... “Toka haraka sana, hayupo wala hakuna mtu,” alimwambia mama Mei, naye alitoka. Aliingia ndani kwake, akafunga mlango na kwenda chumbani kulala. Alilala kwa muda, alikuja kushtuka kusikia mlango  wake mkubwa ukigongwa tena kama ulivyogongwa akiwa ndani kwa mzee Hewa... “Huyo sasa, acha nikamsikilize,” alisema mama Mei huku akitoka kitandani. Aliamini kuwa, aliyegonga ni Mfaume. Yeye dukuduku lake kubwa ni kutaka kujua, alikuwa ana shida gani... “Mambo?” alisalimia Mfaume baada ya mama Mei kufungua mlango na kusimama akiwa
ameushikilia kwa juu... “Poa...karibu,” alisema mama Mei... “Asante sana...nataka kuongea na wewe...” “Kuhusu nini?” “Mambo fulanifulani...” Kama yapi?” “We niambie uko tayari au la!” “Mh!” aliguna mama Mei, kwani kusema hayuko tayari ni balaa maana hakujua Mfaume alikuwa na mazungumzo gani, akaona afadhali ayasikie kwanza... “Nipo tayari,” alisema mama Mei na kusikilizia... “Naomba tukae basi,” alisema Mfaume... “Wapi?” “Popote pale...” “Karibu,” mama Mei alimkaribisha sebuleni kwake. Aliona ni afadhali akae sebuleni kwake kama mgeni... “Pita tu,” alisisitiza karibu yake mama Mei. Baada tu ya kukaa, Mfaume akaanza kusema... “Anti mimi najua wewe ni mke wa mtu, nawe wajijua pia...” “Najijua ndiyo, vipi?” “Oke...vizuri sanasana...lakini mimi kuna jambo limeniumiza sana nikasema lazima nikwambie ulijue...”
“Jambo gani hilo anko?” “Usiku wa kuamkia leo nani aliingia ndani kwako..?” “Hakuna aliyeingia...” “Anti usinidanganye, mimi ni mtu mzima...kijana mmoja wa mtaani, namjua vizuri sana, aliingia kwako. Nilimwona na ametoka saa kumi na moja alfajiri, pia nilimwona, unataka kukataa nini?” Mama Mei nusura presha impande, kwani aliyoambiwa ni ukweli...ukweli mtupu! Na alijua kama mume wake atakuja kuambiwa, ataamini kutokana na kumwonamwona Jombi nje ya nyumba hiyo. Kwa hiyo ataunga... “Mh! Anko sikia nikwambie... huenda ulifanya utafiti wa kutosha sana...ni kweli, siwezi kukataa. Kweli yule mtu alikuja ndani kwangu akaondoka muda huo, lakini si jamaa yangu...” “Jamaa wa nani sasa?” “Alikuja kuomba hifadhi ya kulala tu...” “Ni ndugu yako?” “Ndiyo...” “Baba Mei anamjua?” “Sina hakika,” alijibu mama Mei, jibu ambalo alijua lilimkera sana Mfaume kwani ukweli anaujua... “Kwa hiyo yule kijana alikuja kuomba hifadhi kwako licha ya kwamba ana kwake kule mbele?” aliuliza Mfaume akijifanya anamjua hata kwa sura kijana huyo kumbe alibahatisha tu... Maneno hayo ya Mfaume yakampa mwanga mpya mama Mei, alijua hana namna ya KUKIMBIA UKWELI huo ambao uliwekwa kama kivuli kwake


 kwake... “Nisamehe sana anko, naomba hilo liweke moyoni mwako. Namjua mume wangu...” “Kwa hiyo ni jamaa yako na si nduguyo?” “Ndiyo,” alijibu mama Mei kisha akaangalia chini kwa aibu ya kike, ya usaliti ilhali yeye ni mke wa mtu... “Da! Sasa anti, mimi kawaida yagu siwezi kukaa na dukuduku moyoni...itakuaje? Maana msema ukweli ni mpenzi wa Mungu, lazima nitamwambia mume wako, baba Mei. Mama Mei alishuka chini, akapiga magoti kwenye kapeti na kumwomba sana Mfaume... “Please anko, nifichie siri hiyo, naomba sana niko chini ya miguu yako, nitaachika mimi,” alisema akilia mama Mei. Mfaume alimkazia macho huku akimeza mate ya mahaba kwa namna ambavyo, mama Mei alikuwa akionekana muda huo. Mzigo ulikuwa mzigo kwelikweli, kiuno kiuno kwelikweli, paja paja paja hasa! Si mchezo..! “Utanipa zawadi gani ili nikutunzie siri hii?” aliuliza Mfaume kwa sauti ya kukoroma huku akilegeza macho...
MRUNZI: IRENE MWAMFUPE NDAUKA

No comments