Header Ads

Kanga Moja Kiunoni... Mbengembenge -17


ILIPOISHIA : “Utanipa zawadi gani ili nikutunzie siri hii?” aliuliza Mfaume kwa sauti ya kukoroma huku akilegeza macho... TAMBAA NAYO MWENYEWE... MAMA Mei alishtuka, akamwangalia kwa uso wa hamaki... “Anko, yaani kunitunzia siri hii tu unataka zawadi jamani?! Haya niambie wewe unataka zawadi gani?” “Mimi nimetokea kukupenda sana anti, hiyo ndiyo zawadi yangu pekee kwako,” alisema Mfaume akiangalia pembeni kwa aibu kwani kwa mwanamke kama mama Mei kumwambia nakupenda huku unamkazia macho ilihitaji uso wa kuchunwa! “Sasa na mimi nisemeje hapo? Sijajua,” alisema mama Mei huku akionekana kukasirikia tukio lile... “Ujibu, si umeshajua nina maana gani anti?” “Wala mimi sijajua maana yako...” “Sikia anti, nimesema nipe zawadi ili nikutunzie siri...sasa zawadi ninayoitaka mimi, nakupenda. Kwa hiyo naomba kuwa na wewe japo kwa siku moja tu, basi,” alisema Mfaume akijifanya ana uso wa mbuzi, hana aibu, anampa mtu shua... “Mh! Wapi! Siwezi kuwa na wewe hata kwa nusu siku mwenzangu... wewe kama unataka umwambie tu mume wangu, litakalotokea na litokee na kama ni kuachika niachike kwani naamini mimi sitakuwa wa kwanza kuachika hapa chini ya jua,” alibwabwaja mama Mei... “Haya, nashukuru sana,” alisema Mfaume akisimama na kutoka. Alitoka kwa uangalifu mpaka ndani kwake, akafikia kukaa kwenye kochi kubwa, akajilaza na kuanza kumfikiria mwanamke huyo, kwamba anapata wapi ujasiri wa kumwambia maneno kama yale kwamba, yu tayari kuachika... “Ina maana mimi sina sifa ya kuwa na yeye ila yule jamaa aliyemuingiza... “Lakini pia, ina maana ni mwanamke wa aina gani katika kizazi hiki ambaye haogopi ndoa, haogopi mwanaume, amuogopi mume wake?” alijiuliza Mfaume na kukosa raha. Moyoni alijiuliza, akirudi mume wake amwambie asimwambie? *** Jombi, akiwa kwenye shughuli zake, alimkumbuka mama Mei na jinsi alivyojidhalilisha mbele yake, akaamua kumpigia simu ili eti amwombe msamaha... “Halo,” alipokea mama Mei... “Vipi mzima mama?” alisalimia Jombi... “Mzima ndiyo, unasemaje?” “Nataka kukuomba msamaha kwa yaliyoto...” simu ikakatwa... “Daa!” aliumia Jombi baada ya kukatiwa simu, akajua imetoka hiyo, ikirudi ni pacha! Mama Mei alisonya mwenyewe kisha akasema moyoni...
“Mimi sina haja ya wanaume suruali. Mwanaume unafika kitandani unalala kama mzoga bwana...lo!” Aliachana na huyo na kuanza kumuwaza Mfaume. Alikumbuka maneno waliyozungumza wakiwa wote sebuleni pale... “Ujibu, si umeshajua nina maana gani anti?” “Wala mimi sijajua maana yako...” “Sikia anti, nimesema nipe zawadi ili nikutunzie siri...sasa zawadi ninayoitaka mimi, nakupenda. Kwa hiyo naomba kuwa na wewe japo kwa siku moja tu, basi...” “Mh! Wapi! Siwezi kuwa na wewe hata kwa nusu siku mwenzangu... wewe kama unataka umwambie tu mume wangu, litakalotokea na litokee na kama ni kuachika niachike kwani naamini mimi sitakuwa wa kwanza kuachika hapa chini ya jua...”  “Haya, nashukuru sana...” “Potelea mbali, aseme asiseme atajua mwenyewe. Kwani ana ushahidi gani kwamba kuna mwanaume aliingia na kutoka ndani kwangu?” mama Mei alijipa moyo. *** Siku ile ilipita, muda mwingi mama Mei alikuwa ndani kwake, kwani kuna kila kitu, choo, bafu, stoo na vikorokoro vingine. Jioni ya siku hiyo, mumewe alimpigia simu na mazungumzo yao yalikuwa hivi... “Halo sweet...” “Mzima mama Mei..?” “Mi mzima baby, vipi wewe huko?” “Mzima...aa natarajia kuondoka huku kesho asubuhi, nitafika huko Dar usiku...” “Ah! Sawa darling, lakini nimekumisi kweli mwenzio...” “Ee! Sawasawa...poa basi,” alisema baba Mei na kukata simu. Mama Mei alianza kutetemeka, kwani mazungumzo ya mume wake yaliashiria kwamba, hakuwa sawa... “Kuna kitu, kwa vyovyote vile... baba Mei hawezi kuongea na mimi halafu asitumie jina la upendo...halafu namwambia nimemmsi anasema sawasawa badala ya kusema na mimi pia baby, lazima kuna jambo... “Au Mfaume ana namba yake ameamua kumwambia akiwa hukohuko Kenya?” aliwaza moyoni mama Mei, akakosa raha kabisa. Alijiongeza kwa mawazo mengi mpaka basi. Ilikuwa saa moja juu ya alama usiku, mama Mei akajitanda kanga juu na chini, akatoka kwa umakini hadi kwenye mlango mkubwa wa Mafume, akaushika, akausukuma, ukafunguka, akaingia na kumkuta Mfaume amakaa sebuleni kwake akiangalia tivii... “Karibu sana anti,” Mfaume alikaribisha kwa sauti ya chini ya kuibia wengine wasisikie... Je, nini kilitokea hapo? Usikose kusoma, Jumatatu ijayo.

No comments