Header Ads

Kanga Moja Kiunoni... Mbengembenge-19

 
ILIPOISHIA: “Anko...anko...anko,” aliita mama Mei kwa sauti iliyojaa haraka kama vile kuna jambo baya amelisikia au amelijua wakati huo wakiwa bado wanaendelea kucheza... “Mmm...mmm,” aliitikia Mfaume kwa sauti nzito ya kiume akisubiri kuambiwa alichoitiwa kwa haraka kiasi kile... SASA JIACHIE MWENYEWE... “UTANIACHA ANKO?” eti ndiyo lilikuwa swali la mama Mei... “Wewe tu anti...” “Mimi sitaki uniache,” alisema mama Mei akitoka kwenye kushinikizwa na kuwa hiari yake sasa na upendo juu. Sijui alikumbana na kitu gani kutoka kwenye mchezo wa Mfaume mpaka akaanza kubembeleza mahaba kiasi cha kuomba kujua kama ataachwa... “Sikuachi anti.” Mfaume akawa kama amechochewa sasa, alikimbiza ile mbaya mpaka mama Mei akawa anaguna tu na kusemasema maneno yake, alikuwa hoi, aliishiwa nguvu katika mchezo huo, akahisi ameingia katika maisha mengine mapya tofauti na aliyoyazoea kwenye eneo la mahaba. Walinyamaza, wakawa wanahangaika kila mmoja akiisakanya furaha yake ilipo mpaka ikafika mahali, mama Mei akajitoa kama anayesema liwalo na liwe, kwani mume ni kitu gani bwana! Wangapi wana waume zao lakini hawajatulia! Kwa Mfaume, ilikuwa ni historia nyingine kabisa kwani aliamini bahati ya kumpata mwanamke kama mama Mei, hasa kutokana na uzuri wake wa sura na umbo ni sawasawa na kufanikiwa kumpata malkia wa nchi yenye neema katika zama za dunia ya zamani zile. Chumba walichokuwemo, kwa upande wa dirisha, liliangalia eneo ambalo hakuna mtu aliyekuwa akiweza kupita, kwa hiyo kelele zozote zile, hakuna aliyekuwa na uwezo wa kuzisikia. Lakini mama Mei aliuliza kwanza kabla ya kuanza kuimba... “Baby kuna watu nje ya dirisha huko hawawezi kutusikia?” “Hakuna, kuna uchochoro hautumiwi, upande  wa pili ni godauni la mahindi,” alisema Mfaume kwa tabutabu kwani alikuwa kazini wakati huo. Kusikia vile, mama Mei alijichia kama mtu anayefukuza ndege kwenye shamba la mpunga, kila mara kelele, mara aende kona ile, mara arudi huku. Ikafika mahali akaachia ishara moja kwamba amemaliza safari yake ya upendo kwa mwanaume huyo, akapokelewa, wakapokeleana. Dakika nne nzima hakuna aliyekuwa akisema kitu, kila mmoja alikuwa akihema kwa kasi ya mchoko. Shughuli ilikuwa pevu
sana. Mwishowe, ndiyo mama Mei akasema... “Asante sana baby, nimeinjoi, sijui wewe.” “Hata mimi pia sweet, nakushukuru sana. Nimefarijika sana kuwa na wewe, kwangu ni kama nimeota ndoto kwamba nimekuwa tajiri wakati ni maskini lakini baada ya kuamka nikakuta ni tajiri kweli,” alisema Mfaume huku akimshikashika mwanamke huyo sehemu mbalimbali za mwili wake... “Lakini nakuomba sana anko, usije ukaitoa siri hii kwa watu. Wa kujua anatakiwa kuwa wewe na mimi tu. Usirogwe hata siku moja, ukamwambia mzee mwenye nyumba,” aliomba sana mama Mei akiwa anamchezea kifua Mfaume. “Haitatokea,” alijibu kwa kifupi Mfaume. Kwa mama Mei alijua mzee Hewa akipata habari, atapasuka na yake na lolote litaweza kutokea, hivyo akaona ni vyema akaziba mapema. Usiku huo, mama Mei ni kama alilala chumbani kwa Mfaume kwani baada ya mapumziko marefu, waliingia raundi nyingine na nyingine, hata walipopitiwa na usingizi, muda ulikuwa umekwenda na wakakoroma. Walishtuka saa kumi na moja na nusu alfajiri baada ya kusikia watu wakizungumzazungumza nje kwa sauti za haraka kuwahi makazini. Mfaume ndiye aliyemwamsha mama Mei ambaye aliamka, akatoka kitandani na kukaa kwanza. Mfaume alimshika mkono mpaka sebuleni, yeye akafungua mlango kuangalia mazingira kisha akamtoa alipoona kuko shwari. *** Kulipambazuka kabisa, jua lilianza kuchomoza, wapangaji wengine katika nyumba hiyo walianza kutoka nje, akiwemo mzee Hewa. Mama Mei tangu arudi kitandani kwake, hakuwahi kupata usingizi tena. Muda mwingi alijikuta akijiwazia mwenyewe na kujiona kama mjinga vile... “Sasa ina maana kwenye nyumba hii tu, nimeshatembea na wanaume wawili, mzee Hewa na Mfaume, ukimjumlisha na mume wangu, wanakuwa watatu, nyumba moja... “Mh! Huu sasa ni uhuni uliopitiliza. Kwa nini lakini? Inakuaje mpaka nafikia hatua hii mbaya,” aliwaza sana mama Mei akashindwa kupata majibu na kuamua kuamka kufanya mambo mengine. Akiwa ndani ya kanga moja na taulo kwa juu yake, mama Mei alitoka uani ambako alikutana na mzee mwenye nyumba, Hewa na mpangaji mwingine wakiwa wanazungumzia tukio la usiku, la mwizi kutimuliwa nyumba ya pili... Je, nini kilitokea hapo? Usikose Jumatatu!

No comments