Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge-14

 
ILIPOISHIA: Mama Mei alicheka, lakini akakatisha kicheko baada ya kusikia mtu akienda uani. Alikuwa yule mpangaji aliyemwona Jombi. JIACHIE MWENYEWE SASA... *** KULIKUCHA kabisa, jua lilikuwa juu ya saa nne asubuhi. Ndani ya nyumba hiyo, baada ya kuondoka wengine kwenda makazini kwao, alibaki mzee Hewa na mama Mei  tu. Mzee Hewa yeye ni mstaafu, yupo tu nyumbani akila mafao! Mzee Hewa aliingiwa na moyo wa kumbaka tena mwanamke huyo baada ya kufanikiwa mara ya kwanza bila kusikia malalamiko au lawama. Lakini aliamini safari hii angefanikiwa zaidi kuliko mwanzo kwani hali ya hewa ya mama Mei asubuhi ile ilikuwa nzuri. Alicheka naye vizuri kule uani. Kwa hiyo, mzee huyo alitoka ndani kwake, akapita kukagua mlango kwa mlango ili kujiridhisha kwamba, hakuna watu wengine kwenye vyumba vyao kwanza kabla hajaenda kumgongea mama Mei. *** Kwa upande wake, mama Mei alijilaza kidogo kwenye kochi kubwa akiwaza kuhusu alichofanyiwa na Jombi usiku
uliotangulia... “Yaani mimi ni mwanamke yeye ni mwanaume, siyo ndugu, tumelala pamoja lakini ameshindwa kufanya chochote. Ama kweli yule mwanaume ni kiboko aisee! Tena mbaya zaidi mimi ndiye nimemtafuta baada ya kuona siku ile baa anajiumauma hata kusema hawezi. Au mdomo zege yule?” alijihoji mama Mei... “Ina maana yeye ameridhika kabisa kuniacha na kiu yangu... mh! Afadhali mume wangu angekuwepo tu haya yote yasingetokea,” aliwaza zaidi mama Mei... “Ngo ngo ngo ngo!” mlango wake uligongwa, mama Mei akashtuka kwani hakumjua mgongaji... “Nani? Karibu,” aliitika mwanamke huyo na kutoka, akafungua mlango wa sebuleni, akakutana na sura ya mzee Hewa... “Karibu mzee Hewa,” alisema mama Mei akisisitiza ukaribisho wake kwa mwenye nyumba yake huyo... “Asante binti...nimekuja kukutembelea...” “Karibu,” mama Mei alisema huku akiwa bado ameganda mlangoni kwake... “Karibu wapi sasa, ndani au hapahapa?” “Kwani we unataka kuingia
ndani kwangu?” “Ndiyo lengo langu ndiyo maana nimesema nimekuja kukutembea.” “Hapana mzee Hewa, kuingia ndani kwangu ni hatari, unataka kufanya kama jana? Haiwezekani,” alisema mama Mei lakini huku dhamira ikimsuta kwamba, anamkatalia mzee huyo lakini Jombi alilala humo mpaka kunapambazuka... “Binti, mara moja tu nataka kuongea na wewe,” alisema mzee Hewa... “Ongea hapahapa mzee Hewa...” “Hapa hapana, nataka ndani kwako.” “Basi mimi sitaki.” Mzee Hewa akaona hakuna njia nyingine zaidi ya kumsukumia ndani mwanamke huyo kisha na yeye kuzama na kufunga mlango ili kufanya yake. Na kwa jinsi alivyomkuta alivyo mama Mei kwa muda huo, mzee Hewa alihamasika sana... “Kwa hiyo?” alimuuliza... “Kwa hiyo haiwezekani mzee Hewa.” Mzee huyo alimwangalia kwa muda mama Mei kisha akamshika mkono na kumlazimisha kuingia ndani kwake... “Noo mzee Hewa, nimesema haiwezekani bwana...”
“Itawezekana tu...yaani nipate tabu wakati raha ipo.” “Hapana mzee Hewa, labda twende chumbani kwako...” “Utakataa wewe.” “Siwezi kukataa bwana, nakuapia siwezi.” “Utatangulia mwenyewe?” “Ndiyo nitatangulia mwenyewe.” Mzee Hewa alimwachia mama Mei kisha akasimama kumwangalia kama kweli atakwenda kwake... “Tangulia sasa kutoka basi ili nifunge mlango,” alisema mama Mei. Mzee Hewa alitoka, akaingia ndani kwake. Alikaa sebuleni, akasikia mlango mkubwa wa kwa mama Mei ukifungwa na funguo, akatupia macho mlangoni kwake, mama Mei akazama mwenyewe bwana... waaa! “Enhe, mzee Hewa unasemaje kwani?” alisema mama Mei huku akikaa pembeni ya mzee huyo kiasi cha kugusana... “Binti, mimi nikikuonaga tu wewe naishiwa nguvu mwenzio. Kwa nini hupendi kunielewa binti?” “Mzee Hewa unavyodhani wewe na mimi tunaendana?” “Kwa sababu ya uzee wangu au?” “Ndiyo, si nitaonekana
nataka kukuua?” “Atakayeona hivyo ni nani?” mzee Hewa aliuliza swali ambalo lilimpa tabu mama Mei kulijibu kwani yeye alitaka maongezi ya siri, sasa wasiwasi wa mama Mei watu wakijua nani atajua na atajuaje? Mama Mei akamtolea macho mzee Hewa, akayarembua f’lani hivi, mzee wa watu akaishiwa nguvu kabisa, akamshika mkono mama Mei, akamvutia kwake. Mama Mei akamwegemea mpaka kwenye mapaja. Kisha akaanza kumchojoa nguo mzee Hewa, moja baada ya nyingine huku akisema... “Lakini mzee hewa inatakiwa kuwa na siri sana kuhusu mapenzi yetu, akijua mtu mmoja, atajua na mwingine na mwingine na mwingine, mwishowe yatafika kwa mume wangu, itakuwa balaa mwenzio.” Mara mlango wa mama Mei uligongwa kwa upole sana. Ilionekana mgongaji hakutaka kusikika na mtu mwingine... “Ngo ngo ngo ngo...” Je, nini kilitokea hapo? Usikose kusoma  Ijumaa, Ijumaa ijayo. 

MTUNZI: Irene Mwamfupe Ndauka 

No comments