Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge -12

 
ILIPOISHIA: “Anko uko wapi?” “Niko huku bondeni, kuna baa inaitwa Mundu...” “Nakuomba njoo nyumbani...” SASA ENDELEA NAYO... “MH! Anti kuna nini?” aliuliza Jombi akihisi kwamba, huenda namba yake kwenye simu ya mwanamke huyo imenaswa na mume wake, sasa akambana na kumwambia amuite... “Wewe njoo, utajua hapahapa nyumbani kuna nini!” “Mh! Oke...nije nyumbani kabisa au kwa nje hapo?” “Njoo nyumbani kabisa, ndani tena. Ukifika mimi utanikuta nje nakusubiri.” “Mmh! Anti lakini kwema kweli?” “We njoo tu.” “Oke nakuja.” Jombi aliomba aongezewe bia mbili, alijua anakokwenda kuna ishu kama siyo tukio, lakini hakuwa tayari kulikwepa kama mwanaume! Hivyo aliamini kwamba, kwa kulewa angeweza kukabiliana na lolote mbele ya safari... “Hizo bia mbili lete kwa mpigo halafu miminia na
kiroba kwa juu,” alisema Jombi akimwambia mhudumu... “Sawa.” Ndani ya dakika kumi, Jombi alikuwa sawasawa kiakili kwa maana kwamba, sasa alilewa. Hesabu ya harakaharaka ni kama alipiga bia tano na viroba vitatu...piga picha hapo! Njiani, Jombi alipigiwa simu tena  na mama Mei, akaipokea haraka sana... “Haloo...” “Umefika wapi anko?” “Niko njiani nakuja, kwema lakini?” “We njoo tu,” alisema mama Mei na kukata simu. Jombi alijiridhisha kwamba, kuna kitu kikubwa kule kwa mama Mei kwani kila akimuuliza kwema, anajibiwa wee njoo tu! alitaka kukatisha safari lakini moyoni akasema... “Nikifika nitasimama kwanza nje, akiniambia niingie ndani nakataa. Kama ni shida aniambie palepale nje.” Alipofika nje ya nyumba hiyo, Jombi alitaka kumpigia kwanza simu mzee Hewa na kumsimulia kisa hicho, lakini akajipa ujasiri na kuamua kumpigia mama Mei mwenyewe... “Uko wapo anko?” “Nje hapa.”
“Nakuja.” Jombi alisimama kwa tahadhari kubwa sana, akatokea mama Mei mwenyewe akiwa amejifunga kanga moja tu, kwa kuikatisha kwenye nido. Mwanga wa nje ya nyumba hiyo japokuwa ulikuwa hafifu lakini aliweza kuonekana sawia kwamba, ndani ya kanga hakuwa na kitu kingine. Jombi alishangaa kumwona mama Mei anatembea mpaka kwenye kona ya nyumba hiyo huku akimuita kwa alama ya mkono, akaenda na yeye... “Anko sikia, naingia ndani na wewe nifuate nyuma yangu, sawa?” “Ah! Noo! Kuna nini ndani kwako?” “Unaogopa nini?” “Siyo bwana! Mumeo yupo?” “Angekuwepo ningekuita? Kaenda Nairobi,” alisema mama Mei akiwa amesimama kimachalemachale akihofia mpangaji yeyote au hata mzee Hewa mwenye nyumba anaweza kutoka... “Kweli?” alihoji Jombi... “Kweli kabisa, we njoo kiaina,” alisema mama Mei akianza kutembea. Kwa nyuma, Jombi alipoona mchezo ukitetemeka,
hakuvumilia, akasema moyoni... “Aaa! Hata kama mume wake yuko chini ya kitanda, mimi naingia tu.” Jombi alimfuata mama Mei, akazama naye ndani kwake, sebuleni. Lakini wakati anazama, mpangaji mmoja ambaye wakati baba Mei anasafiri alimuaga, alishangaa kuona mwanaume akimalizikia kuingia... “Haa! Jamaa si kasafiri, huyu ni nani?” alijiuliza yule mpangaji akiwa amesimama mlangoni kwake. Mama Mei alimwonesha sofa la kukaa Jombi, akakaa. Kisha na yeye, mama Mei akakaa jirani yake na kuanza kusema... “Wewe anko si ulisema umenipenda?” “Ndiyo...” “Basi leo ushindwe mwenyewe. Jamaa amekwenda Nairobi anarudi baada ya siku sita...” “Haa! Kweli?” “Kweli ndiyo,” alisema mama Mei akamsogelea Jombi na kumpelekea kinywa, kilipofika karibu akachomoa ulimi, Jombi akaupokea huku akifumbafumba macho kwa ulevi.
Hata kule nje, mama Mei alipotoka, alipomuona tu Jombi alijua yupo hoi kwa pombe! Walijikuta wapo kwenye denda...denda denda mpaka wakaangukia kwenye sofa jingine kubwa, mama Mei akasimama, akamshika mkono Jombi na kumpeleka chumbani, kitandani pwaa! Hali ya Jombi ilizidi kuwa mbaya kwa mwanga wa taa, akajikuta akipitiwa na usingizi wa moja kwa moja. Mama Mei alijitahidi kumwamsha, wapi! Amsha wee wapi! Akamwacha alale! Saa kumi na moja alfajiri, Jombi alishtuka mwenyewe, pombe zilikata sasa, kuangalia hivi ndani ya chumba akagundua yupo ugenini, akakurupuka kutoka kitandani. “Oya...oya! Oyaa,” alimwamsha mama Mei ambaye alilala kifudifudi na kanga aliyoivaa ilivuka yenyewe kwenye kujigeuzageuza. Kwa hiyo alikuwa kama alivyototolewa! Je, Jombi atakwenda? Na je, atakutana nan nini huko? Usikose kusoma Ijumaa,

No comments