Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge-13

 
ILIPOISHIA : “Oya...oya! Oyaa,” Jombi alimwamsha mama Mei ambaye alilala kifudifudi na kanga aliyoivaa ilivuka yenyewe kwenye kujigeuzageuza. Kwa hiyo alikuwa kama alivyototolewa! SASA ENDELEA... “KUMEKUCHA mimi naondoka,...da! Pombe hizi jamani!” alilalamika Jombi. Mama Mei akiwa na hasira zake kwa kukosa mechi, alijigeuzageuza bila kuitikia aga ya Jombi. Alitoka kitandani, akafungua mlango na kumtaka Jombi asubiri kwanza yeye aangalie hali ya hewa ya wapangaji wengine nje ndipo aondoke... Kufunguliwa kwa mlango wa mama Mei kulimkurupusha yule mpangaji mwanaume ambaye alishuhudia mwanaume akiingia
ndani kwa mwanamke huyo. Alitoka kitandani na kusimama sebuleni kwake akisikilizia nini kitaendelea. Mama Mei alipoona hali ya nje ni salama, alirudi ndani, akamtoa Jombi akimtakia maisha mema... “Kwani jioni si tutaonana baby?” aliuliza Jombi... “Uonane na nani? We nenda bwana,” alisema mama Mei kwa sauti iliyojaa hasira. Jombi alipoondoka, mwanamke huyo alifunga mlango mkubwa na kurudi chumbani kwake. Kwa yule mpangaji, akitumia dirisha lake la mbele aliweza kumwona Jombi na kubaini ndiye aliyetoka kwa mama Mei lakini hakumjua kwa sura kutokana na hali ya giza... “Yule ni nani? Siyo Mashaka kweli? Hapana, Mashaka hana tabia za kihuni, atakuwa Madee. Lakini hapana, Madee yupo Uganda,” alisema mpangaji huyo akijitahidi kuwafananisha watu anaowajua yeye na Jombi. *** Kitandani, mama Mei alilala kwa hasira sana. alimshangaa Jombi kulewa kiasi cha kulala kama mfu huku yeye akiwa na usongo ile mbaya... “Wanaume kama wale ndiyo wanaosababisha wake zao wasaliti ndoa. Pombe gani zile sasa? Hanioni tena kumtafuta,” alisema mama Mei akiusaka usingizi mwanana. *** Jombi aligonga dirisha la chumbani
kwake, mkewe akamuuliza... “Wewe nani?” licha ya kwamba alijua mumewe hajarudi... “Aaah! Swali gani hilo mke wangu...” “Lazima niulize kwani kuna ubaya?” “Hakuna ubaya, ungefungua kwanza basi...” “Kwani unatoka wapi muda huu?” “Fungua nitakwambia.” Jombi na mkewe walibishana huku kukiendelea kupambazuka kiasi cha kuwafanya baadhi ya majirani kubaini linaloendelea kwa wawili hao... “Hata siku moja hujawahi kunirudia asubuhi hapa, leo iweje? Mbaya zaidi simu unayo na mimi simu ninayo, nimekupigia sana hujapokea, unadhani mimi nitafurahia tabia hiyo?” mke wa Jombi alikuja juu... “Kumbe unajua sijawahi kurudi asubuhi hata siku moja, ndiyo ujue kuna tatizo mke wangu, fungua basi... mpaka majirani wajue bwana...” “Hata wakijua kuna nini? Na kuna faida gani mimi kuzuia majirani kujua wakati naumia?” Mwishowe, ubinadamu ulimwingia mkewe, akatoka kumfungulia mlango, ikabaki kesi ya ndani. *** Kulikucha, mama Mei akiwa ndani ya kanga moja tu, alikuwa akifanya usafi uani. Kijua kilipokuwa kinatoka, kiliufanya mwili wake uonekane sawia licha ya kuwa ndani ya kanga hiyo moja.
Muda mwingi, kanga ilibughudhiwa na upepo kiasi cha kumfanya yeye awe anaiweka sawa kwa kuibana katikati ya miguu mara kwa mara kisha kuendelea kufagia. Aliyetoka uani asubuhi hiyo na kukutana na mama Mei ni mzee Hewa. Bosi mwenye nyumba..! “Hujambo binti?” mzee huyo alisalimia kwa sauti ya kizee huku akimwangalia mama Mei kwa macho yaliyojaa mahaba ya hali ya juu. Hakujua kama Jombi alilala pale na alichemsha... “Sijambo, shikamoo mzee Hewa...” “Unataka kuninyima nini mpaka unaniamkia?” alisema mzee Hewa kwa sauti yenye utani kidogo... “Sasa jamani kwani mi nimesema nitakunyima nini? Mbona sijakunyima chochote na wewe unajua...” “Basi nisalimie vingine...” “Haya...umeamkaje baby?” alisema mama Mei huku akiachia tabasamu pana... “Nimeamka salama mpenzi wangu, sijui wewe?” mzee Hewa alisalimia kwa furaha huku akiachia tabasamu lenye kushusha ngozi ya mashavuni. Mama Mei alicheka, lakini akakatisha kicheko baada ya kusikia mtu akienda uani. Alikuwa yule mpangaji aliyemwona Jombi. Je, nini kilitokea hapo? Usikose kusoma Jumatatu hii

MTUZI:Irene Mwamfupe Ndauka

1 comment: