Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge -15

 
ILIPOISHIA I: Mara mlango wa mama Mei uligongwa kwa upole sana. Ilionekana mgongaji hakutaka kusikika na mtu mwingine... “Ngo ngo ngo ngo...” TAMBAA NAYO MWENYEWE... “Mh! Nani tena huyo?” aliuliza mama Mei akiwa ameegemea kifua cha mzee Hewa... “Kwani anagonga mlango gani?” mzee Hewa naye aliuliza... “Kwangu...” “Subiri niende nikamchungulie,” alisema mzee Hewa huku akitoka kitandani... “Uwe makini sana baby,” alisema mama Mei huku akiwa na wasiwasi mkubwa kwamba ni nani ingawa alijua si mume wake. Mzee Hewa alikwenda kusimama mlangoni kisha akachungulia nje kupitia tundu la funguo. Aliweza
kumwona mtu aliyesimama kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani kwa mama Mei. Ni mwanaume lakini alionekana kwa tabu. Ilibidi mzee huyo atege macho vizuri ili aweze kumuona sawasa... “Haa! Si Mfaume yule?” alijihoji mzee huyo. Mfaume ni yule mpangaji aliyeshuhudia Jombi akiingia na kutoka asubuhi. Sasa alikuwa anataka nini kwa mama Mei labda ndiyo swali kuu lakini pia je, hakwenda kazini kwani? Hilo nalo lilikuwa swali la msingi... “Anataka nini kwa mama Mei?” alijiuliza mzee Hewa. Alirudi chumbani mbio... “Vipi, ni nani?” mama Mei aliwahi kumuuliza... “Mfaume...” “Mfaume! Ana shida gani na mimi?” “Sijui, mimi ndiyo nikuulize wewe,” alisema mzee Hewa akionesha kushangaa sana. Mama Mei alitaka kutoka kitandani, lakini mzee huyo akamzuia... “Sasa unataka kwenda wapi?” “Nataka nikahakikishe...” “Utahakikishaje?” “Si nitamchungulia.” Mama Mei alikwenda hadi sebuleni, akachungulia na kweli alimwona Mfaume amesimama bado mlangoni pake na anaendelea kugonga mlango
wake kwa umakini sana. Alirudi chumbani kwa mzee Hewa... “Sasa huyu anataka nini?” aliuliza... “Mimi sijui, unajua wewe,” alisema mzee Hewa akiwa amelala kitandani. Mama Mei alifikia kukaa tu akiwa amepoteza muwashawasha wa kuwepo kitandani na mwaume huyo. Alifikiri mengi lakini alikosa majibu ya wazi. Ilifika mahali alitamani angekuwa ndani kwake ili atoke amsikilize lakini ilikuwa haiwezekani tena kutoka, angepita wapi! “Njoo basi mrembo,” mzee Hewa alisema huku akimshika mkono mama Mei na kumvutia kwake. Mama Mei alielekea kwa shingo upande maana mawazo hayakuwa pale. Mzee Hewa kwa ubishi hivyohivyo, alimshikashika mwanamke huyo huku akimbusubusu kiaina sehemu mbalimbali za mwili kwa lengo la kumuweka sawa waanze mchezo. Mama Mei alitekwa na ujanja wa mzee huyo, alisahau kabisa kama Mfaume amesimama mlangoni kwake akigonga, akalegea kwa mzee Hewa, shughuli ikaanza, wakaingia uwanjani. Mzee Hewa licha ya uzee wake bwana, alitumia uwezo wa akiba kummudu mama Mei. Alikumbuka mapozi mbalimbali na kumshirikisha ambapo mwanamke huyo alishangaa kupata kitu roho yake inapenda! Kelele zilikuwa nyingi akimkubali mzee Hewa na mambo yake yote huku lakini akimsisitiza kutoanika siri za penzi lao kwa mtu yeyote na
kumuahidi kumlindia penzi kwamba, hakuna mwingine atakayelipata zaidi ya mume wake, baba Mei tu. Kwa upande wake, mzee Hewa kwa vile alijua kwamba alikoshwa na wowowo na umbo zima la mama Mei alikuwa akicheza huku akimwangalia kama mtafiti wa wanyama anavyokagua ili kupata tiba sahihi. Wakati wa kumaliza shoo, wote walipoteza akili na kuweweseka japo walijitahidi sana kuhakikisha sauti zao hazitoki ndani ya chumba walichokuwemo mpaka wote wakanyoosha mikono na miguu kwa pamoja..! Sasa walichoka, wakawa wamelala kwa mapumziko huku mama Mei akiwa na uso wa aibuaibu ya mbali maana walitoka kwenye tukio la historia. Mzee Hewa alijiona ni mshindi si wa mechi za mchangani, bali ligi kuu kabisa. *** Mama Mei na mzee Hewa walisimama mlangoni wakiangalia uwezekano wa kutoka kwani aliyekuwa akigonga mlango alikuwa kama ameondoka mlangoni hapo... “Ngoja nitoke mimi halafu wewe utafuatia ili nikaangalie mazingira kwanza,” alisema mzee Hewa... Je, nini kilitokea hapo? Usikose  Jumatatu ijayo.

No comments