Header Ads

Kidoa afulia, akosa mkwanja wa bethde

VIDEO Queen mwenye figa matata Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’, wikiendi iliyopita ilikuwa bethdei yake na inadaiwa alijigamba kuwa angefanya bonge la pati lakini cha ajabu ilipita akiwa kajifungia kwao, Kinondoni jijini Dar. Shosti wake wa karibu alimtonya paparazi wetu kwamba, Kidoa aliwaalika ili siku hiyo wale, wanywe lakini cha ajabu ilipofika siku yenyewe akazima simu.
 


“Mwenyewe alidai angefanya bonge la pati, tukajiandaa lakini cha ajabu siku ilipofika hata hewani hakuwa akipatikana, baadaye tukaambiwa mkwanja aliokuwa akiutegemea kufanyia sherehe hakuupata hivyo alishinda nyumbani kwao tu,” kilidai chanzo hicho.

 Katika kujua ukweli wa habari hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Kidoa na alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli niliahirisha kufanya pati lakini si kwa kukosa pesa, ni kwa kuuheshimu Mwezi wa Ramadhani, ukipita nitawaalika jamani

No comments