Header Ads

Kidoa ajiweka kwa kigogo


VIDEO QUEEN Bongo ambaye pia ni msanii wa Bongo Muvi, Asha Salumu ‘Kidoa Akadumba’ amewataka wasanii wanaommendea kukaa chonjo kwa kuwa ana mtu wake (kigogo serikalini jina kapuni) anayemuweka mjini na kujituliza kwake.

Akibonga machache na Showbiz Xtra, Kidoa aliyewahi kuripotiwa kuondoka nyumbani kwa mama yake, Kinondoni jijini Dar na kuhamia kuishi na kigogo huyo maeneo ya Tabata, alisema kuwa mtu huyo ana malengo naye hivyo hana muda kuhangaika na mapenzi ya mastaa.

“Wapo wasanii wengi wanaonifukuzia ila mapenzi yao ya mauzo tu wenye upendo wa kweli wachache, sihitaji stress hata kidogo yaani msanii anayejipa moyo kwamba atakuja kuwa na mimi afute fikra hizo, nimetulia na mwanaume wangu sababu tunapendana na anakidhi mahitaji yangu,” alisema Kidoa.

No comments