Header Ads

Lil Ommy wa Times FM na Shamimu Mlacha wa ITV wafunga ndoa

Mtangazaji wa kituo cha redio cha Times FM, Omary Tambwe Alhamis hii amefunga ndoa na mwanahabari mwenzie, Shamimu Mlacha ambaye ni mtangazaji wa kituo cha runinga cha ITV.
97cd9a0f-c607-440d-ae62-1e796e1a40ed
Wawili hao wamekuwa pamoja kwa miaka kadhaa sasa na wamefunga ndoa ya Kiislamu. Ijumaa hii watakuwa na sherehe kubwa itakayohusisha ndugu, jamaa na marafiki.
c65d6a69-5155-4f4f-92e6-75dc268775b2
“Feels good man,” Ommy ameiambia Bongo5. “In life kama kijana, kama mtu ambaye umejitambua kuna hatua muhimu za maisha lazima upitie, ndoa ni jambo jema hasa kwa imani ya kidini yangu pia ni baraka.”
“Najisikia poa sana especially kuwa na mtu ambaye ana sifa zote za kuitwa mke, mtu ambae ana misingi ya kidini. Allah atuongoze katika hatua hii muhimu na inshallah kwa uwezo wake na dua za ndugu, jamaa na marafiki tutakuwa na ndoa njema yenye upendo na utulivu.”
e267e222-6ffe-4673-9ccc-985e16283cb9 (1)
“Kama kijana kuna muda ambao hutakiwa ukupite na ni muda wa kutulia kuanza kupanga na kujenga familia, kuwa na watoto kuitwa Baba. Actually kutulia kufocus kwenye maisha ya sasa na baadaye. Muda uliopotea haujirudii so ni vema kufanya jambo kwa muda wake. Ni vema pia kufanya mapema kujipenga zaidi,” ameongeza Ommy.
Tunawapongeza Mr and Mrs Omary Tambwe kwa ndoa yao. Tazama picha zao zaidi.
0ab2a522-d5fb-45ff-89c6-05473c5a8ac5
b6577d57-9d36-4dc4-b458-7f90432dd139

CHANZO: BONGO 5

No comments