Header Ads

Madaha Siwezi kuzaa na ‘mwanaume suruali

 
MWANAMUZIKI ambaye pia ni muigizaji, Baby Joseph Madaha amefunguka kuwa anaweza akafikisha hata miaka 40 bila kupata mtoto kwa kuwa hataki kuzaa na ‘mwanaume suruali’. Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi kwa sasa, Madaha alisema bado yupoyupo na itamchukua muda mrefu kuingia kwenye maisha ya ndoa na kupata mtoto kwa kuwa, wanaume wengi ni matapeli wa mapenzi. “Wanawake wengi wanakimbilia kupata watoto au kuolewa bila kujali wanazaa na nani, wanaolewa na nani, mimi bwana bora nizeeke bila mwanaume wala kuitwa mama lakini siwezi kuthubutu kuzaa na mwanaume suruali. “Mwanaume atakuzalisha, utafurahi kuitwa mama lakini matokeo yake unapata tabu ya kulea mwenyewe, ya nini kujipa presha?” alisema Madaha ambaye kwa muda mrefu haijulikani anadate na nani.

No comments