Header Ads

Mama Diamond anywea kwa Zari ..Kisa kipo hapa!


Mama Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’,
Stori: Mayasa Mariwata, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Imevuja! Baada ya muda mrefu kusambaa kwa habari kuwa mama wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’, ‘haivi’ na mwandani wa msanii huyo, Zarinnah Hassan ’Zari The Boss Lady’, imedaiwa kuwa kwa sasa bi mkubwa huyo amenywea kwa kumkubali Zari.
ZARIIMpenzi wa Diamond, Zarinnah Hassan ’Zari The Boss Lady’
Taarifa hizo zilizopenyezwa na chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya familia ya Diamond zimeeleza kuwa, hivi karibuni mama Diamond amesalimu amri na kutamka hadharani kuwa Zari ni kiboko kuliko wanawake wote ambao mwanaye amewahi kuwa nao.
“Mama Diamond kanywea kwa Zari na wala hana lolote la kusema, unajua Zari kamtuliza sana Diamond! Si kama alivyokuwa huko nyuma. Huwezi amini juzikati mama Diamond katamka kabisa kwamba hakuna mwanamke kama Zari maana amemtuliza Diamond vilivyo,” kilichonga chanzo hicho.
diamondDiamond
Baada ya kuunyaka ubuyu huo wa motomoto, Risasi Jumamosi lilimpandia hewani mama Diamond ili kumsikia anazungumziaje ubuyu huo ambapo baada kuelezwa kila kitu bi mkubwa huyo alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“Eeeh mwanangu…eee..”
Risasi Jumamosi liliendelea kumpigia simu mama Diamond baada ya kukata lakini hakuweza kupokea tena.
Zari na mama Diamond wamedaiwa kuwa katika msuguano wa chinichini kutokana na kutoelewana tabia na kila mmoja kutomzungumzia mwenzake kwa mazuri hivyo kwa mama Diamond kudaiwa kusema anamkubali mkwewe huyo, ni dhahiri kwamba amekubali yaishe!

No comments