• Latest News

  July 30, 2016

  Mama: Mimba Ya Jokate Hainihusu

  Jokate Mwegelo ‘Jojo’
  Stori: Boniphace Ngumije na Mayasa Mariwata
  Mama mzazi wa mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Jojo’, Benadertha Ndunguru amefungua kinywa chake kuwa, mimba inayosemekana mwanaye anayo haimuhusu.
  Safu hii ya BMM ilitia maguu nyumbani kwa akina Jokate, maeneo ya Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar ili kuthibitisha ‘kitumbo’ cha mrembo huyo ndipo bi mkubwa huyo alipofunguka hilo baada ya kukosekana kwa Jokate.
  jokateJokate na mama yake mzazi.
  “Jokate amesafiri na anatarajia kurudi siku ya Ijumaa (Jana),” alisikika mama Jokate. Alipoulizwa kuhusu mwanaye kuwa mjamzito ndipo alifunguka;
  “Mimba yake mimi hainihusu, hayo mambo si nyie ndiyo mnayaandika, kwa hiyo mna ukweli nayo au jaribuni kumtafuta mwenyewe na kuzungumza naye,” alisema mama huyo na hata alipobanwa zaidi alikataa kufunguka zaidi ya kufunga geti na kutokomea ndani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mama: Mimba Ya Jokate Hainihusu Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top