• Latest News

  July 26, 2016

  MAN UNITED YAONDOKA CHINI BAADA YA MECHI YAO VS MAN CITY KUAHIRISHWA  Kikosi cha Manchester United kimeondoka Beijing nchini China baada ya mechi yao dhidi ya Man City kuahirishwa.

  Mechi ya Man United dhidi ya Man City ilikuwa ipigwe jana lakini ubovu wa Uwanja wa Bird Nest ulioharibika kutokana na mvua za mfululizo ilisababisha mechi hiyo kuahishwa.

  Man United wameondoka Beijing wakiongozwa na kocha wao mpya, Jose Mourinho ambaye ameikosa mechi hiyo dhidi ya mpinzani wake mkubwa, Pep Guardiola anayeinoa Man City.

  MECHI ZIJAZO ZA MAN UNITED:
  Julai 30 - Manchester United vs Galatasaray, Gothenburg, Sweden
  Agosti 3 - Manchester United vs Everton, Old Trafford

  Agosti 7 - Manchester United vs Leicester, Community Shield, Wembley 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAN UNITED YAONDOKA CHINI BAADA YA MECHI YAO VS MAN CITY KUAHIRISHWA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top