Header Ads

‘Matiti ya Kajala, dawa za Kichina zinahusika’Baada ya gumzo kubwa kuibuka juu ya muonekano mpya wa matiti ya msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja, shostito wake wa karibu amemwaga ubuyu kuwa, dawa za kuongeza matiti za Kichina zinahusika.
Akipigia stori na Ijumaa hivi karibuni, mtoa ubuyu wetu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, huko nyuma matiti ya Kajala yalikuwa ‘ndala’ akawa anatumia dawa f’lani za kupaka ili kuyafanya yatune.
“Nyie muoneni vile tu lakini zile nido zake za sasa Mchina anahusika sana, hawezi kuanika ukweli lakini habari ndiyo hiyo,” alisema mtoa ubuyu huyo.
Paparazi wetu alibahatika kuongea na Kajala juu ya madai hayo ambapo alisema: “Watu bwana wanaongea sana, je nikiamua sasa kutumia hizo dawa itakuwaje? Niseme tu kwamba matiti yangu ni orijino na siku zote yana mvuto ndiyo maana sionagi hatari kuyaanika.”

No comments