Header Ads

Mchina amshushia kipigo Mtanzania hadi kifo

MCHINA MAUAJI GEITA (1)Mr. Swii akimshushia kipigo kijana Elisha adi kukatisha uhai wake.
Kijana mmoja aliyejukikana kwa jina moja (Elisha) mkazi wa Kabindi Mkoani Geita amefariki Dunia baada ya kupigwa na mchina kwa jina “Mr. Swii” kwa madai ya kwamba alilalamika ili wapandishiwe ongezeko la mshahara. Taarifa zinadai waliopigwa wengine wawili wako hospitali kwa matibabu zaidi.
MCHINA MAUAJI GEITA (2)Marehemu alipopigwa akaenda Hospitali na baada ya hapo aliambiwa arudi kazini huku hali yake ikiwa mbaya na ndipo alipodondoka na kuzimia na wakafanya jitihada ya kumpeleka hospitali ya Mkoa kabla ya kufariki Dunia.
MCHINA MAUAJI GEITA (3)Tukio hili limetokea katika Mgodi wa Nyamahuna uliopo Katoro Mkoa wa Geita. Mgodi huu unachimba Dhahabu na Shaba.
Mashuhuda wanasema kuwa “Mr. Swii” pamoja na walinzi wa Mgodi huo ndio waliohusika katika kuwapiga Wafanyakazi hao na kupelekea mfanyakazi mmoja kufariki Dunia kwa Kipigo hicho.
CREDIT: JF

No comments