• Latest News

  July 26, 2016

  MFANYABIASHARA ALIYEKUWA AKIJIINGIZIA MILIONI SABA KWA DAKIKA APANDISHWA TENA KIZIMBANI

  Mfanyabiashara anayetuhumiwa kujiingia fedha zipatazo shilingi milioni saba kwa dakika, Mohamed Mustafa Yusufali amepandishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar kusomewa mashtaka yanayomkabili.
  Yusufali na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali, yakiwemo udanganyifu, kughushi, kukweka kulipa kodi na kutakatisha fedha haramu pamoja na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 15.6.

  Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Mashauri, ameiahirisha kesi hiyo mpaka Alhamisi ya Julai 28, 2016, baada ya upande wa mashtaka kudaiwa kuwa na upungufu katika hati ya mashtaka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MFANYABIASHARA ALIYEKUWA AKIJIINGIZIA MILIONI SABA KWA DAKIKA APANDISHWA TENA KIZIMBANI Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top