Header Ads

Miss Tabata Apatikana Kwa Kishindo West Park, Dar

Miss Tabata 2016 (10)
Miss Tabata mwaka 2016,  Grace Malikita akiwa kwenye kiti chake baada ya kuibuka mshindi
Miss Tabata 2016 (9)
..akiwa na mshindi wa pili (kulia) Nasra Munna na wa tatu Mariam Maabadi.
Miss Tabata 2016 (1)
Mmoja wa wahusika akitangaza washindi walioingia Tano Bora
Miss Tabata 2016 (2)
Washidni waliofanikiwa kuingia Tano Bora wakiwa kwenye pozi.
Miss Tabata 2016 (3)
…wakichangua maswali
Miss Tabata 2016 (6)
Miss Tabata alipongezwa na mrembo aliyemkabithi taji
Miss Tabata 2016 (9)
HATIMAYE ule mtanange uliosubiriwa wa muda mrefu na wakazi wa Tabata jijini Dar katika kumpata mrembo atakaye wawakilisha katika Mashindano ya Miss Ilala mwaka 2016, mlimbwende Grace Malikita aibuka kidedea.
Grayce, jana usiku katika Ukumbi wa Dar West Park uliopo Tabata aliwabwaga chini warembo wengine 15 na kuwa mshindi wa Miss Tabata mwaka 20016 huku nafasi ya pili ikishikwa na Nasra Muna na nafasi ya tatu ikienda kwa Mariam Maabadi.
Kinyanganyiro hicho kilihudhuriwa na wapenda urembo kibao sambamba na burududani ya kukata na mundu kutoka kwa Tanzania African Stars ‘Twanga Pepeta’ wakiongozwa na Luiza Mbutu, Kalala Junior, Haji Ramadhani, Khalid Chokoraa na wengineo.
(Habari/Picha:  Gabriel Ng’osha/GPL)

No comments