Header Ads

Mo Music anasa ‘kimalovee’ kwa Baby J wa Zanzibar

MKALI wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ anadaiwa kunasa ‘kimalovee’ na msanii mwenzake, Jamila Abdallah ‘Baby J’ ambaye muda mwingi makazi yake ni Zanzibar, lakini mara kwa mara wamekuwa wakionekana kujiachia maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na wasanii hao kilieleza kuwa, hiyo ndiyo kapo mpya ya mjini licha ya kuwa, hawajaamua kuweka wazi uhusiano wao kwa mashabiki lakini si siri tena sababu hata wasanii wenzao wengi wanafahamu.

Jamila Abdallah ‘Baby J’
Baada ya kuupata ubuyu huo, mtandao wa Global Publishers ilimvutia waya Baby J ambaye aliruka vikali na kudai ni mtu wake wa karibu tu, upande wa pili Mo Music alipotafutwa alianza kwa kuangua kicheko na kusema kuwa;
“Kweli mjini mtu hakunyimi umbeya sijui mmeyapataje haya, sioni cha ajabu hapo ila muda ukiwadia nitaweka wazi kila kitu.”

CHANZO: GPL

No comments