Header Ads

Msindai arudi CCM akiwa Dodoma leo

Mgana Msindai (kulia) akiongea jambo.
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na baadaye kuhama chama na kujiunga na Chadema, Mgana Msindai amerudi CCM leo.
CLkG9v5UYAEMLK6
 Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman  Mbowe alipokuwa akimkabidhi kadi Mgana Msindai (katikati).
Msindai alitangaza uamuzi huo leo mjini Dodoma baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati anaendesha mkutano mkuu wa CCM uliomchagua Rais Dk John Magufuli kuongoza chama.
Msindai alisema aliamua kurudi CCM baada ya kuona hakuna cha kupinga baada ya Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais wa nchi.
Msindai aliingia Chadema baada ya aliyekuwa mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa kujiunga na Chadema mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu.

No comments