• Latest News

  July 05, 2016

  Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry leo Atangaza kuwa kesho Jumatano ni Sikukuu ya Eid el Fitri

  Kwa kipindi cha mwezi sasa waislamu walikuwa katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakitimiza  ibada ya nguzo za uislamu ambayo ni Kufunga.
   
  Baadhi ya waislamu kutoka mataifa mbali mbali wakiwepo wajerumani na Afrika magharibi, leo wamesherekea sikukuu ya Eid el fitr baada ya kumaliza mfungo wao.
   
  Hata hivyo leo Mufti Mkuu wa tanzania Zubeir Bin Ally amewataka pia waislam kujitokeza kesho katika misikiti mbalimbali kwa ajili ya ibada ya Eid el Fitr.
   
  Taarifa ambayo imetolewa leo ni uthibitisho wa sikukuu ya Eid el Fitr ambapo Waislam wote walikua wakisubiri kuandama kwa mwezi.
   
  Kwenye taarifa yake Muft Zubeir amesema Mwezi huo umeonekana sehemu mbalimbali za nchi yetu ya Tanzania, hivyo  kesho Jumatano ni Sikukuu ya Eid el Fitri
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry leo Atangaza kuwa kesho Jumatano ni Sikukuu ya Eid el Fitri Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top