Header Ads

Mwanaheri: Adui yangu mkubwa ni uchafu..


Mwigizaji wa Filmu za Bongo, Mwanaheri Ahmed
MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa Mpaka Home! Baada ya wiki jana kuwa na Enock wa ya Moto Band, leo tunaye Mwanaheri Ahmed (23) anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu. Anaishi Kijitonyama, Dar na dada yake. Ni mambo mengi amechonga na safu hii, twende pamoja:
mwanaheri (4)Mwanaheri Ahmed akipanga vitu kwenye jokofu.
Mpaka Home: Vipi mbona umejifungia hivyo?
mwanaheri (5)Mwanaheri Ahmed akiosha vyombo.
Mwana: Yaani mimi nikikaa hivi ndani ndiyo napenda na kama sina kitu cha muhimu cha kunifanya nitoke hata siku tatu naweza kukaa ndani.
 Mpaka Home: Kwa hiyo hata sokoni huendi?
mwanaheri (6)Mwana: Mara nyingi tunanunua vitu vya wiki au mwezi.
Mpaka Home: Kwa jinsi ulivyoumbika, ulishawahi kujifunga khanga moja na kutoka nje?
mwanaheri (7)Mwanaheri akifanya mazoezi.
Mwana: Siwezi kabisa tena kwa mtaani kwetu huku siwezi si unajua vijana watakavyosumbua.
Mpaka Home: Mastaa wengi wanapenda kuamka mchana kweupe na si asubuhi, vipi kwa upande wako?
mwanaheri (8)Mwana: Mimi basi nitakuwa navunja rekodi naamka alfajiri sana na kufanya mazoezi kila siku.
Mpaka Home: Ni vazi gani unalopenda kuvaa unapokuwa nyumbani?
Mwana: Napenda sana kuvaa dera.
mwanaheri (9)Mwanaheri akifanya usafi.
Mpaka Home: Unapenda kufanya nini ukiwa nyumbani?
Mwana: Kupika chakula kitamu.
mwanaheri (10)Mwanaheri akichambua mcehele ili apike.
Mpaka Home: Nini ambacho hukipendi ndani kwako?
Mwana: Yaani adui yangu mkubwa huku ndani ni uchafu hata kama naumwa hoi lazima nifanye usafi kwanza na vingine ndiyo vinafuata.
mwanaheri (2)Mpaka Home: Umeshawahi kumleta mchumba wako hapa unapoishi?
mwanaheri (3)Mwana: Hapana si unajua mimi nimefunzwa, maadili hayaniruhusu.
Mpaka Home: Nje ya kazi ya usanii ni kitu gani kingine unafanya?
mwanaheri (11)Mwana: Mimi ni mjasirimali, natengeneza sabuni nzuri sana za  kufulia na kuoshea vyombo.
Mpaka Home: Nakushukuru sana Mwanaheri
Mwana: Karibu tena nyumbani.

No comments