Header Ads

Nape Azindua Filamu Ya Sikitu Kwa Kishindo jijini Dar!
Wazara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye usiku wa kuamkia leo alikuwa  mgeni rasmi kwenye Uzinduzi wa Filamu ya Sikitu, na kupewa heshima ya kuizindua filamu hiyo ndani ya Ukumbi wa Sinema  uliopo ndani ya jengo la Quality Centter Barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam, ambapo filamu hiyo iliandaliwa na msanii wa tasnia hiyo Kajala Masanja.

Akizungumza kwenye Uzinduzi huo,  Nape alisema  kuwa filamu ya Sikitu, ina ubora unaohitajika kuendelezwa na waandaaji wengine wa filamu hapa nchini, ili ziweze kupata nafasi kubwa zaidi za kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema kama ilivyofanyika kwa filamu hiyo.

Pia Nape aliagiza kuwa kuanzia leo  mtu yoyote atakaye atakamatwa na filamu au kazi ya msanii yoyote hapa nchini na nje ya nchi ikawa haina stakabadhi ya TRA, basi achukuliwe hatua kama wahalifu wengine wa makosa ya uharamia.

“Serikali tumejipanga kusimamia kazi za wasanii kwa ukamilifu, hivyo kuonyesha tumejipanga tutakuwa na operation za  mara kwa mara kwa ajili ya kukamata wale wote wanaohujumu kazi za sanaa yetu na lengo ni kuboresha na kuwafanya wasanii wa nchi hii wanufaike na kile wanachokifanya kutokana na sanaa ya kazi zao,” alisema Nape.


No comments