Header Ads

Nay wa Mitego akamatwa na polisi kisha kuojiwa kwa siku 2 kisa cha yote ni utajiri wake wa ghaflaKimenuka mbaya! Nyuma ya sakata la staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kukamatwa na polisi kisha kuhojiwa kwa siku mbili katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuna madai mengi lakini Wikienda limetonywa kuwa kisa cha yote ni utajiri wake wa ghafla wenye maswali. 

KUKAMATWA KWAKE Ijumaa iliyopita, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilithibitisha kumshikilia rapa huyo lakini halikuweka wazi sababu za kufanya hivyo. 
 
 
TUJIUNGE NA KAMANDA SIRRO Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, ACP Simon Sirro alisema kuwa Nay wa Mitego alihojiwa kwenye Kituo Kikuu (Central) kisha kuachiwa kwa dhamana huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kuhusiana na tuhuma zinazomkabili (hakuzitaja). “Ni kweli tulimhoji Nay wa Mitego na yupo nje kwa dhamana. Kuhusu kukamatwa kwake, nitatoa taarifa kwa nini tulimkamata,” alisema Kamanda Sirro. 
 
WIKIENDA MZIGONI Ili kukata kiu ya maswali ya mashabiki wake yaliyoibuka juu ya kukamatwa kwa Nay wa Mitego, gazeti hili lilizama mzigoni, lengo likiwa ni moja tu kutaka kujua kwa nini msanii huyo aliwekwa nyuma ya nondo kwa siku mbili za Alhamisi na Ijumaa iliyopita. Katika nusanusa, ilibainika kuwa Nay alishikiliwa na
polisi kufuatia utajiri wake mkubwa alionao ili kujua namna alivyoupata na kama alikuwa akilipa kodi. 


MAGUFULI HATANII “Sasa hivi hali ni tete na siyo kwa Nay tu. Hata mastaa wengine matumbo joto maana rungu la polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) halina utani kwa mtu yeyote mwenye utajiri unaotia shaka maana mkuu wa nchi (Rais John Pombe Magufuli) ameashaagiza jambo hilo lifanyike bila kujali nani ni nani. “Sasa kwa Nay kama nilivyowaambia kuna vitu vingi lakini kitendo cha kusema kuwa ana utajiri unaozidi shilingi bilioni moja ndani ya kipindi kifupi inatia shaka. 

KISA KUNADI UTAJIRI WAKE “Mara kwa mara Nay amekuwa akihojiwa na kunadi utajiri wake kuwa ana nyumba kadhaa, magari kibao, Bajaj na fungu kubwa lipo benki. “Sasa lazima watu wajiulize kama mkwanja wote huo ameupata kwa muziki huuhuu wa Bongo Fleva? Mbona wapo wasanii wengi Bongo tena wa kitambo lakini hawana utajiri kama huo? 

UTAJIRI WA ZAIDI YA BIL. 1 “Ukiachilia mbali intavyu ya mwanzoni mwa mwaka huu ambapo alisema ana zaidi ya shilingi bilioni moja, hapa katikati amekuwa akinunua magari ikiwemo Range Rover Vogue ambalo aliagiza nje ya nchi lakini akalipiga mnada bandarini. “Pia inasemekana hivi karibuni alinunua nyumba nyingine maeneo ya Kimara
(Dar). Hiyo ni mbali na zile tatu alizozitaja kwenye intavyu. 


ANUNUA NYUMBA, APANGA KUIVUNJA 
“Inadaiwa nyumba hiyo ameinunua shilingi milioni themanini lakini akasema anaivunja ili ajenge gharofa ‘so’ utagundua kuwa hakuwa na shida ya nyumba bali kiwanja kwa ajili ya kujenga ghorofa. 

MAGARI YA NAY “Pia hapo katikati, ukiacha Nissan Murano na Toyota Passo, Nay alinunua Toyota Prado jipya na daladala nyingine za kumwaga kwa ajili ya biashara ya usafirishaji wa abiria jijini Dar. “Nadhani hapo ndipo shaka ilipoanzia kwa sababu ukilinganisha muziki anaofanya ambapo anategemea shoo zinazobipu za mara mojamoja na utajiri wake vinapishana. “Ngoja tusubiri majibu ya uchunguzi wa polisi lakini mbali na mambo mengine, ishu kubwa ni utajiri wa jamaa (Nay),” kilidai chanzo chetu. Lakini kwa upande wake Nay amekuwa akisisitiza kuwa, mbali na muziki ana vitega uchumi ambavyo vinamuingizia kipato ikiwemo daladala, Bajaj, saluni na vinginevyo. 

HUYU HAPA NAY Baada ya kumwagiwa ubuyu huo , Wikienda lilimtafuta Nay ambapo mbali na kukiri kukamatwa, hakuwa tayari kuzungumzia ishu hiyo kiundani kwa madai kuwa ipo chini ya uchunguzi wa polisi na kwamba hatakiwi kuizungumzia. “Ni kweli nilikamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano lakini sitakiwi kuizungumzia ishu hiyo hivyo tusubiri hadi kamanda atakapotoa tamko,” alisema Nay kwa unyonge
CREDIT: IJUMAA WIKIENDA

 SOMA HAPA CHINI....

NAY WA MITEGO AONESHA JEURI YA PESA BONYEZA HAPA

No comments