Header Ads

Neymar; Kiwembe mwingine La Liga mwenye wapenzi wengi!

Neymar-Barcelona
Neymar da Silva Santos Junior.
WIKI kadhaa zilizopita ukurasa huu uliandika habari zinazomhusu winga mshambuliaji wa Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo juu ya msururu wa wanawake aliotoka nao kimapenzi. Lakini kama ulidhani tabia hiyo ni ya Mreno huyo pekee, utakuwa umekosea, kwani katika kikosi cha Barcelona, ambao ni wapinzani wakubwa wa Real, wote wakishiriki Ligi Kuu ya huko maarufu kama La Liga, yupo kiwembe mwingine, raia wa Brazil, Neymar da Silva Santos Junior.
nicole
Nicole Bahls (27).
Neymar ni kiwembe hasa na katika kuthibitisha hilo, alimpata mtoto wake wa kwanza, akiwa na umri wa miaka 19 tu, wakati huo akikipiga na Santos ya nyumbani kwao Brazil.
Akiwa na umri wa miaka 24 hivi sasa, mchezaji huyo mwenye kasi na uwezo wa kuitumia vizuri miguu yake yote katika soka, anafahamika kutoka na wasichana zaidi ya 11 hadi hivi sasa, wengine kadhaa wakiwa ni wakubwa kwake kiumri.
Maira
Maira Cardi, (27).
Ifuatayo ni orodha ya warembo hao; Carolina Nogeira Dantas, muigizaji wa Kibrazil aliyezaliwa mwaka 1993 aliyekutana na Neymar kati ya 2009-2010 na ambaye alimzalia mtoto wa kiume, Lucca 2011. Pia mwanamitindo Barbara Evans wa Brazil naye alitoka na mwanasoka huyo mwaka 2010.
Mwingine ni mwanamitindo ambaye pia ni mwanahabari, Nicole Bahls (27) aliyevinjari na Neymar mwaka 2011, Daniela Carvalho (27) pia, ambaye alikuwa na mchezaji huyo mwaka huohuo. Katika orodha hiyo, yupo pia mwanamitindo Carol Abranches (25) ambaye naye alikutana na nyota huyo mwaka 2011. Muigizaji mwingine, Andressa Suita, mwenye umri wa miaka 21 naye aliingia kwenye 18 za mchezaji huyo mwaka 2013.
andressa-suita-body-decotado
Andressa Suita.
Maira Cardi, (27) alikula maisha ya Neymar mwaka 2011 kabla ya nahodha huyo wa zamani wa Brazil hajaangukia kwa dansa Roberta Appratti (26). Dansa mwingine Mbrazil, Carol Belli (22) naye anahusishwa na uhusiano wa kimapenzi na mshambuliaji huyo wa Barcelona mwaka 2012.
Msichana aliyezaliwa mwaka 1992, Dani Sperle ndiye binti anayetembea na mwanasoka huyu kwa sasa, uvumi ukienea kuwa ndiye mkewe ajaye lakini kabla ya kuwa naye, alivinjari na muigizaji mwingine wa Brazil, Bruna Marquezine aliyezaliwa 1995 na ambao uhusiano wao ulikatika mwaka.
Carol-Abranches-Divulgação
Carol Abranches (25).

No comments