• Latest News

  July 24, 2016

  Olik atajwa mtayarishaji video bora Kenya

  Mtayarishaji wa video za muziki nchini Kenya, Enos Olik, ametajwa kuwa ni bora katika kutayarisha video za wasanii mbalimbali ndani na nje ya Kenya.
  Enos Olik
  Katika watayarishaji watano bora Kenya, Young Wallace, J Blessing, Thomas Mboss, Sammy Dee, Olik ametajwa kuwa ni bora zaidi katika kutengeneza video za kisasa.
  Hata hivyo inadaiwa gharama zake zimekuwa juu tofauti na wengine kutokana na ubora wa kazi zake.
  Olik ameshafanya video za wasanii mbalimbali kama Nishike, Sura Yako, Still The One na Nerea za Sauti Sol, Kioo (Jaguar), Ivo Ivo (Octopizzo), Come Over (Vanessa Mdee), Pamoja (P-Unit) na wasanii wengine wengi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Olik atajwa mtayarishaji video bora Kenya Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top