Header Ads

Penzi la Kiba laibua mtifuano! Sabby atibua ndoto za ndoa ya Jokate, Gigy, Amber wadaiwa kuzichapa

 
Penzi la mwanamuziki aliye kwenye levo za juu, Alikiba Saleh ‘King Kiba’ limeibua mtifuano wa aina yake kati ya ma-video queen ‘hot’ Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ na Lulu Auggen ‘Amber Lulu’, Ijumaa lina ubuyu ulionyooka!
 


KISIKIE CHANZO 
Chanzo chetu kilicho karibu na wanadada hao kilitutonya kuwa, hapo nyuma kidogo, Gigy na Amber Lulu walikuwa mashosti walioshibana waliokuwa wakiishi pamoja lakini walikuja kuzinguana hadi kufikia hatua ya kuzichapa kisa kikiwa ni penzi la Kiba. “Unajua kuna wakati Gigy alikuwa karibu sana na Kiba na ikadaiwa kuwa wanatoka, hata Gigy aliwahi kusema yule ni mtu wake. Kwa kipindi hicho Gigy na Amber Lulu walikuwa wakiishi pamoja. Sasa kuna wakati Amber Lulu alikuwa akionekana maeneo na Kiba, Gigy akainasa. “Unaambiwa siku moja wakiwa geto kwao walibaruana ile mbaya, eti Gigy alikuwa akimtuhumu mwenzake kuwa anamzunguka kwa Kiba. Kuanzia hapo ndiyo ushosti ukaisha,” kilinyetisha chanzo hicho.
 
 GIGY, AMBER LULU WAGEUKA PAKA NA CHUI Ilidaiwa kuwa, licha ya kwamba kutifuana huko kulikuwa ni kipindi hicho wakati Gigy akidai kutoka na Kiba, hivi karibuni wawili hao walikutana na wakaanzishiana tena ambapo kama siyo kuamuliwa yangetokea mengine. “Hata sasa wakikutana ni kama paka na chui, kubaruana nje nje, kisa cha yote hayo eti ni kugombea penzi la Kiba, hivi yule Kiba ana nini mpaka anasababisha songombingo kwa mademu?” Alihoji mtoa habari huyo. AMBER 

LULU AMWAGA MBOGA
 Katika kuthibitisha kuzinguana kwa ‘wauza nyago’ hao, hivi karibuni, Amber Lulu alikiri kutoiva na Gigy akianika wazi kuwa, chanzo ni penzi la Kiba.
“Mimi siko sawa na Gigy, alikuwa rafiki yangu na ni kweli nilikuwa naishi naye geto kwangu lakini kwa sasa kila mtu kivyake. Sababu ni Kiba, wakati nakaa naye kuna wakati alikuwa yuko na Kiba halafu akahisi namzunguka, hapo ndipo kikanuka,” alisema Amber Lulu. 


MSIKIE GIGY Akizungumzia kutifuana kwake na Amber Lulu, Gigy aliyewahi kukiri kuwahi kutoka na Kiba alisema hawezi kumzungumzia kwa kuwa alichomfanyia hakikustahili kufanywa na yeye. “Nikimzungumzia sana nitakuwa nampa kiki (umaarufu) tu lakini mwenyewe anajua alichonifanyia siyo poa,” alisema Gigy akisisitiza kuwa hataki kumzungumzia mrembo huyo. SABBY AMTIBULIA JOKATE
Wakati Kiba akiwafanya Gigy na Amber Lulu kutaka kutoana roho, inadaiwa kuwa mrembo mwingine ambaye ni Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sabrina Omary ’Sabby Angel’ naye amesababisha ndoto za mwanadada Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kuolewa na Kiba kuzimika baada ya kubainika ameingilia penzi lao. Ilidaiwa kuwa, mara baada ya Sabby kuibuka na kudai Kiba ni wake wakati watu wakijua mwenye mali si yeye, Jokate alianza kurudi nyuma na kuona kama mpenzi wake huyo waliyekuwa wamepanga kuja kuwa mke na mume ameanza kumsaliti, hivyo akaona ni heri akae pembeni. “Ndiyo maana mara baada ya Sabby kuibuka, Jokate akawa anamkwepa Kiba na hata alipotakiwa kuzungumzia uhusiano wao alikuwa akitoa majibu ya kuonesha amekata tamaa ya kuolewa na Kiba,” alisema msanii mmoja wa filamu ambaye yuko karibu na Jokate.


 MTUNGO WA KIBA NI HATARI Kufuatia kuibuka kwa warembo mbalimbali na kudai walikuwa wapenzi wa Kiba, Ijumaa limebaini kuwa, msanii huyo wa Bongo Fleva, licha ya kwamba havumi kwenye ‘mambo hayo’ lakini yumo, mtungo wake na warembo unaweza kuwa wa hatari kukaribia ule wa hasimu wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Mpaka sasa Kiba amedaiwa kutoka na Elizabeth Michael ‘Lulu’, Sabby, Gigy, Amber Lulu, Jokate, achilia mbali wale watoto watatu aliozaa kwa mama tofauti.

 KIBA SIYO MSEMAJI Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Kiba kuzungumzia ‘situwesheni’ ya kusababisha songombingo kwa warembo sambamba na mtungo wake lakini kama kawa, simu yake iliita bila kupokelewa. Hata hivyo, mara nyingi Kiba siyo msemaji hasa linapokuja suala la maisha yake binafsi na ndiyo maana kila uhusiano wake wa kimapenzi unakuwa wa siri.

CHANZO: IJUMAA

No comments