Header Ads

Pombe kali zitamuua Wolper huku akidaiwa kupewa mimba na mpenzi wake Harmonize!


WOLPER (2)

Dar es Salaam: Msanii ‘hot’ wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anaonekana kubobea kwenye unywaji wa pombe kali huku kukiwa na madai kuwa, mpenzi wake, Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’ amemtundika mimba, jambo ambalo ni hatari kwa afya yake.
Hilo limekuja kufuatia juzikati staa huyo kunaswa tena akiwa anakunywa pombe iliyodaiwa ni kali alipokuwa kwenye Shoo ya Black Tie iliyofanyika kwenye Ukumbi wa King Solomoni, Namanga jijini Dar.                                      CHANZO: GPL
WOLPER (1)
Watu wa karibu wa staa huyo wanaeleza kuwa, mara nyingi wamekuwa wakimuona mdada huyo akiwa anakunywa pombe kali, hali ambayo inaweza kuwa ni hatari kwa maisha yake.
“Yaani Wolper pombe anazokunywa zitammaliza, sijui kama anaweza kupitisha siku bila kunywa na mbaya zaidi sasa anagida zile pombe kalikali, kwa kweli namsikitikia sana,” alisema rafiki wa karibu wa staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina.
shilole wolper (10) Akaongeza: “Hata siku ambayo msanii mwenzake, Shilole (Zuwena Mohammed) alipofuturisha, Wolper alitinga akiwa na glasi yenye pombe, hali iliyowafanya wengi kuchukulia kwamba ‘mitungi’ ni sehemu ya maisha yake.
“Mbaya zaidi kuna hizi taarifa kuwa ana mimba, sasa ikiwa hivyo ni wazi yanaweza yakamkuta kama yaliyompata shosti wake Wema Sepetu (Wema inadaiwa kutumia pombe kali ni moja za sababu ya mimba yake kutoka).”
Akizungumzia unywaji wa pombe wa Wolper huku ikidaiwa ni mjamzito, dokta mmoja wa hospitali ya serikali iliyopo jijini Dar aliyetambulisha kwa jina moja na Dokta Makere alisema:
WOLPER (3)“Unywaji wa pombe kali hasa kwa mwanamke mwenye mimba ni hatari, kwa hali kama hiyo ya Wolper kuzaa itakuwa ngumu, labda abadili mfumo wa maisha yake.
“Iko hivi, matumizi ya pombe kwa wajawazito husababisha watoto kuzaliwa wakiwa na uwezo mdogo wa akili (mataahira) lakini pia pombe inaweza kuharibu mimba na kusababisha itoke kabla hivyo ni vyema akina mama wawe makini na hilo.”
WOLPER (4)Mwandishi wetu alizungumza na Wolper siku aliponaswa pale King Solomoni ambapo alisema haoni shida katika hilo kwani anatambua anachokifanya.
“Hapa usione hivi, nimeanzia mbali ni muendelezo tu na wala sioni shida,” alisema Wolper huku akionekana ‘kapendeza’ ile mbaya.
Alipoulizwa kwa nini anapigia ‘tungi’ wakati inadaiwa ana mimba, staa huyo alionekana kutompatiliza paparazi wetu na kumtaka amuache afanye yake.
WOLPER-21.jpg

No comments