Header Ads

Rais Magufuli Achaguliwa Rasmi Kuwa Mwenyekiti wa CCM, Dodoma...Video ipo hapa akiongea

Leo Jumamosi, July 23, 2016 ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi(CCM) kumthibitisha Rais John Magufuli ili awe mwenyekiti mpya wa chama cha mapinduzi kumpokea kijiti mwenyekiti anayeng'atuka, Rais mstaafu, Dokta Jakaya Kikwete.
Wajumbe wengi wako ukumbini tayari kusubiri mkutano uanze rasmi, tuwe sote pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Dodoma.
======

KIKAO CHA JIONI
Watu wamesharejea tayari kwa kumalizia ngw'e ya mwisho ya mwisho ya mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi ikiwemo kutangazwa kwa matokeo ya kura zilizopigwa kumuidhinisha mwenyekiti wa chama.

Mpendazoe: Baada ya kuona anayoyafanya Rais Magufuli, narudi rasmi CCM.

 • Nilipoingia CHADEMA, nilijaribu kutoa mawazo yangu, sifa ya kupata uongozi CHADEMA ni kupigwa na kulala rumande.
 • Mtindo wa kupokezana kijiti ni mfano mzuri wa kuigwa, nashukuru sana kwa kunipa nafasi, mimi narudi CCM.
Msindai: Ninaomba msamaha kwa wanachama wote wa CCM walionikwaza na mimi nimwewasemehe, nilipokwenda ni kama mahabusu.

 • Kona zote kashika Magufuli, Anatupeleka mahala tunapostahili na nawaomba wanaCCM wenzangu tuwe na Rais wetu.
 • Magufuli akishakua mwenyekiti, aingie na kwenye chama kwani kina rasilimali nyingi ili tufike salama.
 • Rais wetu, sisi tunang'atuka, nampongeza kwa kuchagua vijana. Nikaona aibu, nikasema nitarudi CCM kwa baba na mama.
 • Wale wadokozi muda wao umekwisha hata ndani ya chama.
Kikwete: Ningeshangaa sana(Msindai) ungekaa muda mrefu kule, hufanani nako, hufanani nao

 • Wanacheza mchangani, Mtu uliwahi kuwa waziri mkuu, sasa unagombea uenyekiti wa wilaya, sijui yeye na Kubenea atashinda nani!

Magufuli kapitishwa kwa kura zote 2398 zilizopigwa, hakuna kura ya hapana.

Kikwete: Ndugu John Pombe Magufuli amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi

Magufuli

 • Magufuli: Leo ni siku muhimu kihistoria kwa maisha yangu na chama chetu kwa ujumla.
 • Magufuli: Naamini nitaweza, mimi sio mgeni katika chama, niko kwenye chama takribani mika 40, kamwe sitawaangusha.
 • Magufuli: Hata baada ya kunichagua kupeperusha bendera ya Rais, hamkuniacha peke yangu.
 • Magufuli: Tunafahamu uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa na ushindani mkubwa, sina cha kuwalipa kwa ushirikiano mlionipa kwenye uchaguzi.
 • Magufuli: Naomba niwashukuru angalau wachache kwa kuwataja majina, siwezi kusahau mchango mkubwa wa Ali Hassan Mwinyi.
 • Magufuli: Mzee Mwinyi ndio aliongoza kamati kuu, iliyonichagua mimi kugombea ubunge jimbo la Biharamulo, angenikata ningeishia hapo.
 • Magufuli: Namshukuru mzee Mkapa kwa kuniteua waziri mwaka huo huo nilipoteuliwa mbunge.
 • Magufuli: Namshukuru mzee Kikwete kwa kuniteua kusimamia wizara mbalimbali na kusimamia mchakato wa mimi kuteuliwa kugombea Urais.
 • Magufuli: Mzee Kikwete uliendelea kukaa kimya japo ulitukanwa kwa sababu yangu, sina cha kukulipa.
 • Magufuli: Mzee Kikwete ulinipigia simu mara nne kunitaka kuchukua uenyekiti, nilikataa kwa kuanzisha point nyingine.
 • Magufuli: Ukatukanwa kwa kushikilia uenyekiti, moyo wako ni wa kipekee. Moyo wako wa uvumilivu sina hakika kama nitaweza kuvumilia.
 • Magufuli: Siku unaingia kwenye mkutano, alafu ukakuta watu wanaimani na mtu fulani, siku hiyohiyo robo hata nusu wangepotea.
 • Magufuli: Nikiuuliza moyo wangu kilichokutokea kama kingenitokea, sijui ingukuwaje.
 • Magufuli: Nawashukuru pia mzee Mangula, wajumbe wa kamati kuu na mkutano mkuu mliopitisha jina langu.
 • Magufuli: Chama chetu ni kikongwe nchini, Afrika na duniani kwa ujumla. Takribani miaka 40 ya uhai wake kimepata mafanikio mengi.
 • CCM imeendelea kuongoza dola, kinaaminiwa Afrika na duniani kote na kimeendelea kulinda na kudumisha muungano wetu.
 • CCM Kimeendelea kuongoza dola, kinaaminiwa Afrika na duniani kote na kimeendelea kulinda na kudumisha muungano wetu.
 • Nitaendelea kuulinda muungano kwa nguvu zangu zote.
 • CCM Hatupaswi kubweteka kwani tuna kazi kubwa ya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo. #JFLeo
 • Tukishindwa kutatua changamoto na kufikia matarajio ya wananchi, tutapoteza mvuto.
 • Natarajia kufanya mambo yafuatayo, kwanza kuimarisha utendaji kazi wa chama.
 • Mwalimu alisema chama legelege kinazaa serikali legelege, CCM ndio bosi wa mabosi wote waliopo serikalini.
 • Atakaeshindwa kujua ndani ya serikali yangu kuwa mabosi zake ni CCM, ajiandae kuondoka.
 • Kuondoa vyeo vyote visivyokuwa na tija hasa wakati huu.
 • Kuna haja ya kutumia mtoto wa miaka minane kuwa chipukizi badala ya kumuacha asome?
 • Tunawazuia wanaCCM wengine kupata vyeo kwa sababu ya madaraka yetu tuliyonayo, wanaCCM tuwe mfano wa kuongoza mabadiliko.
 • Nafahamu ili watendaji wafanye kazi vizuri lazima wawe na maslahi bora, sitopenda kuona watendaji wetu wanakuwa omba omba.
 • Nafahamu chama chetu kina rasimali nyingi, tutaonda kikosi kazi kutambua mali zote za chama na zinatumikaje.
 • Nafahamu chama chetu kina rasimali nyingi, tutaunda kikosi kazi kutambua mali zote za chama na zinatumikaje.
 • Tutahimiza wanachama kulipia ada za uanachama tena kwa njia ya kielektroniki.
 • Tutaongeza idadi ya wanachama, washabiki na wapenzi, siasa ni mchezo wa idadi.
 • Katika kipindi cha uongozi wangu, nitashirikiana na nyie kuhakikisha tunaliondoa tatizo la rushwa.
 • Kikwete hukua rafiki wa rushwa, ungekua mla rushwa, mimi nisingekuwa Rais, ule wao wataukula rushwa nikiwa mwenyekiti.


==========
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na Rais Magufuli pamoja na wake zao wameshaingia ukumbini, wamo pia Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na marais wastaafu wa serikali ya muungano.

Mkutano umeanza kwa kuimba wimbo wa taifa na kinachoendelea kwa sasa ni wimbo wa chama cha mapinduzi kumuaga mwenyekiti anayeng'atuka, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Anaeongea sasa ni katibu mkuu wa chama cha mapinduzi, AbdulRahman Kinana ambae anaelezea sheria iliyoitisha mkutano mkuu na wajumbe wanaotakiwa kuhudhuria ni kuanzia theluthi mbili ya wajumbe wote lakini wajumbe waliofika ni asilimia 99.4 na anamkaribisha mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi.

Anaeongea kwa sasa ni mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na anatambulisha waliohudhuria na kuwashukuru wote walioandaa mkutano na waliohudhuria.

Kikwete: Nimeambiwa hali ya usalama ni nzuri na ya uhakika. Tumealika watu mbali mbali ikiwemo mabalozi na viongozi wa vyama vya siasa, kuja kwao ni jambo la heshma na tunawaomba muendelee ushirikiano na chama chetu kitarudisha maradufu upendo mliotuonyesha kwetu.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1990, Mwl Nyerere alipong'atuka na kumuachia mzee Mwinyi, mara ya pili ilikuwa Juni 1996 alipong'atuka mwenyekiti Mwinyi na kumuachia Mkapa na Juni 2006 nilikabidhiwa, leo zamu yangu.

Tulifanya kazi ya ziada kumshawishi Rais Magufuli awe mwenyekiti wa chama, nilipomwambia mara ya kwanza mwezi February aliniambia yeye hana haraka na mimi niendelee. Nadhani kunifanya niachane na hayo mazungumzo, akanikaribisha ugali na baada ya kula tukaagana.

Urais ni ofisi kubwa sana, siku hizi mimi nalala, usingizi unaisha. Mzee usingizi hauishi. Majibu ya Rais Magufuli hayakunishangaza kwani hata mimi nilipoambiwa mara ya kwanza nilimkatalia mzee Mkapa lakini baadae mazungumzo yalifanyika.

Tofauti ya wakati ule na sasa, hakukuwepo vyombo vya habari na watu waongo na wafitini. Hakukuwepo na wakati wowote wa mimi kukataa, wakageuza eti mimi sitaki kutoka, wanataka wanihukumu mimi kwa uongo wao.

Safari yangu ilianza Aprili 1975 nilipowasili Singida kuwa katibu msaidizi wa TANU mkoa wa Singida na mwaka mmoja baadae nikapelekwa jeshini, nikaenda Zanzibar na kupawa dhamana ya kuandaa mfumo mpya upande wa Zanzibar, nilihuzika kuandaa mchakato wa kupata viongozi wa chama. 1980 nilihamishiwa ofisi ndogo ya makao makuu Dar es Salaam, 1981 nikaenda Tabora, 1983 nikarudishwa jeshini, miaka mitatu baadae nikahamishiwa Nachingwea. Mwaka 1988 nikamaliza kwenye chama na kuwa mbunge na kuteuliwa naibu waziri wa nishati na madini na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.

Nitaendelea kuwa mwanachama wa kawaida kwenye tawi la kijiji changu cha Msoga na nitaendea kutoa ushauri kupitia baraza la wazee. Natoa shukraan kwa mwenyezi Mungu, pili nawashukuru wazazi wangu kwa kunizaa, kunilea na kunisomesha mpaka kupata mafanikio maishani. Namshukuru mzee John Mhavile(Marehemu), yeye ndie aliekuwa mwenyekiti wa jopo kunisahili na kuniona nafaa kwenye chama. Pia alikuwepo mzee Butiku na Pius Msekwa. Namshukuru mzee Pius Msekwa aliekuwa mtendaji mkuu wa kwanza CCM kwa mambo mengi ikiwepo kunipa dhamana kubwa nikiwa na umri mdogo wa miaka 26.

Natoa shukrani zangu za dhati kwa wazee wawili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, yeye ndie aliyenifanya nijulikane kwa watanzania. Wa pili ni mzee Benjamin Mkapa, namshukuru kwa kuniamini na kunipa dhamana ya kuongoza diplomasia Tanzania kwa miaka kumi mfululizo, iliniwezesha kuijua dunia na watu mbalimbali duniani na ilinisaidia sana katika uongozi wangu nilipokuwa Rais.

Sina kitu wala namna ya kuwalipa mzee Mwinyi na mzee Mkapa kwa waliyonitendea maishani, nawaombea maisha marefu.

Mheshimiwa Kikwete kamaliza kutoa hotuba yake ya kuaga na kumaliza kwa kumshukuru mke wake, mama Salma Kikwete na kumshukuru kwa kuwa ana mchango katika kipindi chote cha mafanikio yake pia amewashukuru wanawe na wajukuu zake kwa kumkosa baba na babu yao pia kwa kuwa wahanga mara kadhaa kutokana yeye kuwa mwana siasa.

Anaeongea kwa sasa ni mzee Yusuph Makamba, Makamba amesema

 • Kikwete anachukia ufisadi kiasi cha kumkata rafiki yake kipenzi, Lowassa.
 • Askofu Gwajima alisema uongo, kisha anamsingizia Jakaya kuwa amekataa kumuachia Magufuli.
 • Pengo la jino la dhahabu Jakaya Kikwete linazibwa na jino lingine la dhahabu Magufuli.
 • Kocha anaondoka lakini hatuachi peke yetu, anatuachia kocha alietupa ushindi uchaguzi ulioupita.
 • Alichosema Magufuli, amekataa vimemo ikiwemo changu, kuna tofauti kati ya vimemo na ushauri na ushauri wangu ameukubali.
 • Jakaya aliwabatiza kwa maji, Magufuli atawabatiza kwa moto.
Sasa wajumbe wa mkutano mkuu wanapiga kura ya NDIO au HAPANA kwa mwenyekiti aliyependekezwa Rais John Pombe Magufuli.

Kwa sasa ni mapumziko baada ya zoezi la upigaji kura kumalizika, wakirejea kutakuwa na utangazaji wa matokeo ya kura.

No comments