• Latest News

  July 07, 2016

  Rais Magufuli Amteua Deogratius Ndejembi Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Kongwa Mkoani Dodoma

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

  Uhamisho wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.

  Bw. Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  07 Julai, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli Amteua Deogratius Ndejembi Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Kongwa Mkoani Dodoma Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top