• Latest News

  July 09, 2016

  Rais Magufuli Amteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS)


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).

  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 07 Julai, 2016.

  Kabla ya uteuzi huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).

  Dkt. Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu tarehe 30 Juni, 2016.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  08 Julai, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli Amteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top