Header Ads

Samatta atupia, aikaribia Man United

 
MSHAMBULIAJI Mtanzania Mbwana Ally Samatta, juzi usiku aliiongoza timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kusonga mbele katika hatua ya tatu ya Michuano ya Europa, ambapo alifunga penalti iliyochangia mafanikio hayo. Licha ya kuwa Genk ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya Budućnost Podgorica ya Montenegro, bado kina Samatta walisonga mbele kwa kuwa katika mchezo wa awali Genk ilishinda mabao 2-0, hivyo kufanya matokeo kusomeka mabao 2-2, baada ya kukamilika kwa dakika zote ndipo hatua ya penalti ikatumika kuamua matokeo. Mafanikio hayo yanaifanya Genk kuingia raundi ya tatu na kama itasonga mbele itaingia hatua ya mtoano kisha ikifanikiwa hapo itatinga hatua ya makundi ambapo huko ndipo itakapokutana na timu vigogo zikiwemo Manchester United, Inter Milan na Fiorentina. Katika mchezo wa juzi Genk ilishinda kwa penalti 4-2, ambapo wafungaji wa Budućnost walikuwa ni Risto Radunović na Radomir Djalovic, wakati wafungaji wa Genk ni Thomas Buffel, Bryan Heynen, Samatta na Dries Wouters. Katika hatua ijayo, Genk itacheza na Cork City ya Jamhuri ya Ireland, mechi ya kwanza ikitarajiwa kuchezwa Julai 28, na kurudiwa Agosti 4, 2016.

No comments